Home » Matokeo

Category Archives: Matokeo

ORODHA YA WANAFUNZI WAPYA WALIOPANGIWA KIDATO CHA TANO 2017

MABADILIKO YA SHULE KWA WANAFUNZI WA TAHASUSI YA
PCB WALIOCHAGULIWA KWENDA MADIBIRA SEKONDARI NA
WALIOPANGWA UPYA MADIBIRA SEKONDARI TAHASUSI YA
CBG
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefanya mabadiliko ya kuwapangia shule
wanafunzi 56 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule
ya Sekondari Madibira Tahasusi ya PCB na kuwapeleka katika shule
zingine zenye tahasusi (Combination) hiyo ndani ya Mkoa wa Mbeya na
Mikoa ya jirani. Mabadiliko haya ni kwa sababu maalum. Majina na shule
mpya walizopangiwa wanafunzi hao inapatikana kwenye tovuti ya
http://www.tamisemi.go.tz
Aidha, wanafunzi wapya 56 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano
katika shule ya Sekondari Madibira Tahasusi ya CBG kama inavyoonekana
kwenye tovuti tajwa.
Wanafunzi hawa wanapaswa kuripoti katika shule walizopangiwa tarehe
17 Julai, 2017.
IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
OFISI YA RAIS -TAMISEMI.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WANAFUNZI-WALIOCHAGULIWA-KIDATO-CHA-TANO-MADIBIRA-SEKONDARI-2017

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2O17/18

TAKWIMU MUHIMU:
Jumla ya watahiniwa wa shule – 349,524
wasichana – 178,775 (51.1%)
wavulana – 170,749 (48.9%)
Jumla ya watahiniwa wa kujitegemea – 47,751
wasichana – 24,587 (51.5%)
wavulana – 23,164 (48.5%)
Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu – 96,018 (27.60%)
VIGEZO VILIVYOTUMIKA KWA MWAKA HUU:
i) AAA hadi CCD kama cut off point kwenye masomo ya tahasusi (Combination)
ii) Credit 3 na pointi zisizopungua 25 kwenye Daraja
iii) Machaguo yaliyojazwa na mwanafunzi kwenye selform.
iv) Nafasi zilizopo katika Shule husika
WANAFUNZI WENYE SIFA
Kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi 93,019 ndio wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama nilivyoainisha hapo juu.
Kati ya hao, Wanafunzi 92,998 ni wa Shule (School Candidates) na Wanafunzi 21 walisoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
TAREHE YA KURIPOTI
Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2017, utaanza tarehe 17 Julai 2017

lakini kwa wanafunzi wanaongia Kidato cha Sita watafungua Shule tarehe 3/7/2017 kama ilivyokuwa

imepangwa. Kwa kuwa upangaji wa wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kwa mwaka 2017 umezingatia
machaguo ya wanafunzi wenyewe na nafasi zilizopo katika Shule husika, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule. Nitumie nafasi hii, kuwaagiza wanafunzi wote kuripoti katika Shule walizopangwa kwa wakati.
Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi yasiku 14 kuanzia tarehe ya kufungua Shule, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017
inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya: http://www.tamisemi.go.tz & http://www.moe.go.tz
Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya: http://www.tamisemi.go.tz
IMETOLEWA NA:
George B. Simbachawene (Mb)
WAZIRI WA NCHI, OR-TAMISEMI
Fungua link hizi hapa chini kuona majina:

MATOKEO YA RUFAA KWA KIDATO CHA NNE 2016

Fungua kiunganishi hicho hapo chini kuona matokeo ya watahiniwa waliokata rufaa dhidi ya matokeo yao ya awali ya kidato cha nne kwa mwaka 2016

MATOKEO YA RUFAA AWAMU YA I-CSEE 2016

MATOKEO KIDATO CHA PILI (FTNA) NA DARASA LA NNE (SFNA) 2016

examresults

Fuata viunganishi hapo chini

Kidato cha Pili 2016

Darasa la Nne

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA VETA MWAKA 2017

untitled

Kama uliomba kujiunga na chuo chochote cha VETA nchini kwa mwaka 2017, hiki hapa chini ni kiunganishi cha majina yaliyochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo

UCHAGUZI WA MAJINA VETA

%d bloggers like this: