Home » Matangazo

Category Archives: Matangazo

NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Serikali inatarajia kuajiri Walimu 92 wa Shahada na 174 wa Stashahada wa masomo ya Fizikia, Hisabati, Kilimo na Biashara kwa Shule za Sekondari na Walimu 2,767 wa Cheti kwa Shule za Msingi.

Waombaji kwa shule za Sekondari wawe waliohitimu mafunzo ya Ualimu mwaka 2016 au kabla, na wale wa Shule za Msingi wawe waliohitimu mafunzo yao mwaka 2014 au kabla.

Sifa za Waombaji:

 Walimu wa Sekondari:
(i) Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo moja la kufundishia au zaidi au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo moja la kufundishia au zaidi pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali. Masomo ya kufundishia ni kati ya Fizikia, Hisabati, Kilimo au Biashara.
(ii) Stashahada ya Ualimu katika masomo yaliyoainishwa kwenye kipengele Na. 2.1 (i) hapo juu.

(iii) Cheti cha Kidato cha Sita
(iv) Cheti cha Kidato cha Nne

Walimu wa Shule za Msingi:
(i) Astashahada ya Ualimu iliyotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(ii) Cheti cha Kidato cha Nne (wenye cheti Kidato cha Sita watapewa kipaumbele).

Utaratibu wa Kutuma Maombi:

(a) Maombi yatumwe kupitia Posta kwa njia ya Rejesta (EMS). Juu ya bahasha iandikwe kwa mkono “Maombi ya Kazi ya Ualimu – Sekondari au Maombi ya Kazi ya Ualimu – Msingi”.

(b) Mwombaji aambatishe nakala za Vyeti vilivyothibitishwa (Certified) na Mwanasheria pamoja na “Transcript”.

NB: Barua za maombi zisiwasilishwe kwa mkono. Barua zitakazowasilishwa kwa mkono hazitapokelewa.

 Masuala Mengine ya Kuzingatia:
(a) Mwombaji aandike majina yake yote matatu. Kama Vyeti vina majina mawili, utaratibu wa kisheria wa kuongeza jina uzingatiwe.
(b) Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.

Mwisho wa kupokelewa maombi ni tarehe 31/08/2017.

Maombi yatumwe kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
S. L. P. 10,
40479 DODOMA.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

NACTE KANDA YA KASKAZINI WAHAMIA OFISI MPYA

THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION

 (NACTE)

 TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuuhabarisha Umma na wadau wa Elimu nchini hasa wa kanda ya Kaskazini ya kwamba, ofisi ya baraza ya kanda ya kaskazini imehamia katika jengo jipya la NSSF COMMERCIAL COMPLEX (MAFAO HOUSE) ghorofa ya nane (8), jengo hili lipo katika barabara ya Old Moshi, Plot No. 1. Karibu na New Arusha Hotel kuelekea Kibo Palace Hotel.

Kabla ya kuhama ofisi hizo zilikuwa katika majengo ya Arusha Technical College (ATC)Chumba namba nne (4), karibu na njia panda ya barabara ya kuelekea Nairobi (Namanga Road) na ile inayotoka Moshi.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ofisi zetu za Kanda ya Kaskazini kwa anuani zifuatazo;-

NACTE Northern Zone

P.o. Box 14333 Arusha,

Mobile: 0658444556/57

Email: northern.zone@nacte.go.tz

IMETOLEWA NA;

KITENGO CHA HABARI MAWASILIANO

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

3/08/2017

ADA MPYA YA MAOMBI YA UDAHILI KWA VYUO VYA UMMA 2017/18

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ADA YA MAOMBI YA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza linapenda kuvitaarifu Vyuo na Taasisi za Umma zinazotoa mafunzo yanayosimamiwa na Baraza (NACTE) pamoja na Umma kwa ujumla kuwa, Serikali imeagiza kuwa Ada ya Maombi ya Udahili (Admission Fee) inayotakiwa kutozwa kwa mwanafunzi anayeomba Udahili katika Vyuo/Taasisi za umma kwa mwaka wa masomo 2017/2018 isizidi shilingi Elfu Kumi (Tsh. 10,000/=) kuanzia sasa.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 28/07/2017

TAHADHALI KUTOKA CHUO KIKUU DAR (UDSM) KUHUSU TARATIBU ZA UDAHILI

Tumepata taarifa kwamba kuna matapeli wamekuwa wakiwahadaa wanafunzi wanaoomba udahili wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwapa taratibu zisizo sahihi na kisha kuwaibia fedha zao.

Tunaomba kuujulisha umma kwa ujumla kwamba udahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unafanywa kwa kupitia mfumo wa kompyuta katika mtandao maalumu unaopatikana katika tovuti iliyopo kwenye anuani: udsm.admission.ac.tz. Maelezo ya jinsi ya kuomba udahili pamoja na habari nyingine za udahili zinapatikana katika tovuti ya chuo yenye anuani: www.udsm.ac.tz.

Maombi hayapokelewi kwa kujaza fomu. Pili, ada ya maombi ya udahili ni Shilingi 20,000/= tu ambazo zinalipwa kwa kutumia mitandao ya simu kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa kwenye mfumo wa udahili.

Tunatoa pole kwa waliopata usumbufu na tunasisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizo rasmi katika zoezi zima la udahili.

Tunawatakia udahili mwema.

Imetolewa na Kurugenzi ya Shahada za Awali

Simu:       0222410069 AU 0222410751

TAARIFA KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOTAKA KUSOMA CHETI AU DIPLOMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA CHETI AU STASHAHADA  KATIKA VYUO VINAVYOSIMAMIWA NA BARAZA  KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza linapenda kuwataarifu wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwezi Mei, 2017 na umma kwa ujumla; kuwa sasa wanaweza kutuma maombi  ya Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika Vyuo vya Serikali  kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya Udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.


Kwa wale ambao walishatuma maombi na wanataka kuongeza sifa ya kidato cha sita wanaweza kufanya hivyo sasa kupitia kurasa zao binafisi (Profile).Pia baraza linapenda kuwakumbusha na kuwahimiza wote wenye sifa kama zilivyo ainishwa kwenye kitabu cha Muongozo wa Udahili (Admission Guidebook) kinachopatikana kwenye tovuti ya Baraza kuwa, wafanye maombi yao mapema kabla ya tarehe 20 Agosti, 2017 kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sababu hakutakuwa na muda wa nyongeza.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 22/07/2017

%d bloggers like this: