Home » Video

Category Archives: Video

VIDEO: TUKIO LA KUPATWA KWA JUA

Jana tarehe 21 Agosti, baadhi ya maeneo ya sayari ya Dunia yalishuhudia giza la mchana ikiwa ni matokeo ya kupatwa kwa jua (Mwezi kuwa katikati ya Jua na Dunia). Tukio hili ambalo hujirudia kila baada ya mwaka mmoja au miwili na kushuhudiwa na sehemu mbalimbali za dunia kwa kiwango tofauti huvuta hisia za watu wengi na pengine kuzua taharuki kwa wale ambao wanakuwa hawana taarifa au elimu ya mabadiliko hayo ya kidunia.

Elimu Leo tumefanikiwa kupata kipande cha video ya tukio la jana kama ilivyochukuliwa na shirika la safari za anga za mbali la Marekani (NASA) kikionyesha mionekano mbalimbali ya jua katika bara la Amerika ambako kwa mwaka huu ndiko tukio hilo limeonekana vizuri zaidi.

 

COREEN SWAI: BINTI WA KITANZANIA ALIYEBUNI FIMBO YA WASIOONA

Binti wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam Coreen Swai ametengeneza fimbo ya kuwasaidia kutembea walemavu wasioona. Lakini sio fimbo ya kawaida kama zile tunazozijua wengi. Hii ni ya KIPEKEE kabisa kama unavyoweza kuiona kwenye video hapo chini

Chanzo:DW

VIDEO: JPM ALIVYORUDI SHULENI KWAKE

Rais  Dkt John Pombe Magufuli akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari Katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera.
Dkt Magufuli amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo.
Dkt Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo.
Video: Ikulu

Habari kwa hisani ya BBC

SHULE ZA MSINGI KENYA ZAANZA KUFUNDISHA KI-DIJITALI

 

 

 

Zaidi ya shule 17,000 nchini kenya zimepokea vifaa (Laptop) vya kufundishia na kujifunza kwa njia ya ki-dijitali. Mtaala mpya wa elimu nchini humo unaelekeza kutumika kwa vifaa hivyo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili nchini kote na hadi sasa kiasi cha laptop 992,073 zimesambazwa katika shule 17,000 na zaidi ya walimu 95,000 wamepokea mafunzo ya kutumia mfumo huo mpya wa kufundishia.

Sanjali na hatua hizo, viwanda viwili vya kuunganisha vifaa hivyo vimejengwa katika vyuo vikuu vya Jomo Kenyatta na  Moi ili kuharakisha uzalishaji wa vifaa hivyo  vitakavyosambazwa kwenye shule zote za msingi za umma zipatazo 23,951 na kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kukabiliana na ushindani wa kimataifa katika umri mdogo.

Rais Uhuru Kenyetta na Makamu wake, William Rutto wamekagua maendeleo ya mpango huo wa serikali walipotembelea shule ya msingi Kathithyamaa wakati wa kampeni za urais zilizofanyika katika eneo la Machakosi hapo jana Jumanne.

“Tutaendelea kuunga mkono mpango huu wa kujifunza ki-dijitali hadi uzifikie shule zote za umma 23,951. Maudhui ya ki-dijitali yameshaandaliwa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili na wanafunzi hao sasa wanaweza kuyapata kupitia vifaa hivi,” alisema Rais Kenyetta.

Alisema pia shule zote za umma zinaunganishwa na mkongo wa taifa ili kuhakikisha upatikanaji wa mtandao utakaowezesha ukamilifu wa mpango huo. Rais Kenyatta amesema kwa Machakosi pekee, vifaa 25,731 vimesambazwa katika shule 609 kati ya shule 829 zenye miundombinu ya mpango huo ambapo jumla ya Shilingi za kenya Milioni 49.7 zimetumika.

Aidha, Rais Kenyetta ameahidi utoaji wa elimu bure kwa shule za sekondari kuanzia mwaka ujao ikiwa wakenya watamchagua kwa muhula wa pili wa urais.

 

VIDEO FUPI: MWANAFUNZI WA ILBORU ATENGENEZA ROBOTI

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ilboru iliyopo Jijini Arusha akionesha namna ‘Roboti’ alillolitengeneza likifanya kazi.

Kijana huyo ambaye jina lake bado halijapatikana ametengeneza ‘Roboti’ hilo kwa vifaa mbalimbali ambavyo vingi si rasmi kama inavyoonekana kwenye video hiyo.

Chanzo: Jamii Forum.

%d bloggers like this: