Follow Elimu Leo Blog on WordPress.com

Member of The Internet Defense League

Sajili Barua pepe yako upate habari mpya kila zinapotokea

Join 1,637 other followers

Idadi ya waliotutembelea

  • 207,897

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2018

Mkoa wa Dar Es Salaam

Mkoa wa Lindi

Mkoa wa Mtwara

Mkoa wa Morogoro

Manispaa ya Morogoro

Mkoa wa Pwani

Wilaya ya Mkuranga – Wavulana

Wilaya ya Mkuranga – Wasichana

Mkoa wa Arusha

Wilaya ya Meru

Mkoa wa Simiyu

Wilaya ya Bariadi

Halmashauri ya mji wa Bariadi

Wilaya ya busega

Wilaya ya Itilima

Wilaya ya Maswa

Wilaya ya Meatu

Wanafunzi wenye ulemavu

 

Advertisements

UDHAMINI WA MASOMO ULAYA

1. Applications are invited for the newly open call i.e. VLIR-ICP Master
Scholarships at Katholieke Universiteit Leuven in Belgium. The call is open
for Tanzanian students for 2018-2019 academic years.
2. Students can get more information through the given link:
ICP Master Scholarships at Katholieke Universiteit Leuven in Belgium
3. More scholarships are available for Tanzanian Students
NB: VLIR-UOS only provides full scholarships for the total duration of
the training or Master Programes.
The deadline of the scholarship is February 1, 2018.

MLOGANZILA KUDAHILI WANAFUNZI 15,000 WA AFYA NA TIBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi hospitali ya Taaluma na Tiba ya chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi MAMC, kilichopo wilaya ya Ubungo mkoani pwani, amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kuhakikisha wanakamilisha mara moja ujenzi wa mabweni, madarasa na kumbi za mihadhara katika Chuo hicho.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo wakati wa uzinduzi wa hospitali hiyo ambapo amesema tayari serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi huo na kuwa Kati ya fedha hizo tayari kiasi cha shilingi bilioni Nne kimelipwa kwa TBA ili kuanza ujenzi huo na kwamba ujenzi utakapokamilika utawezesha udahili wa wanafunzi 15,000 wa afya na tiba kwa mara moja tofauti na ilivyokuwa awali wanafunzi 4500 Pekee ndiyo walioweza kudahiliwa.

Rais Magufuli pia ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia na wizara ya Afya kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha hospital hiyo inatekeleza majukumu yake kwa weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Wakati wa uzinduzi huo Rais Magufuli amesifu na kupongeza jitihada zilizofanywa na Serikali ya awamu ya Nne chini ya uongozi wake Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete za kuhakikisha eneo la ujenzi linapatikana na ujenzi unafanyika na hatimaye wananchi kupata huduma za afya.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia profesa Joyce Ndalichako amesema uwepo wa Chuo hicho chenye mitambo na vifaa vya kisasa kutalisaidia Taifa kupata wataalamu wenye uwezo ambao itsaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa wataalnu wa afya hapa nchini.

SIMULIZI: TENDA WEMA NENDA ZAKO

KUMBUKA MAISHANI UNAYEMSAIDIA SI LAZIMA AWE NDIYE ATAKAYEKUSAIDIA.


Kwa miaka mingi niliishi nikiamini watu wote wapo kama nilivyo mimi, yaani ukinitendea wema lazima nitatafuta njia ya kukutendea wema, pale ambapo mtu alinitendea wema nikataka kumlipa halafu akakataa, basi huyo alibadilika kuwa ndugu yangu kabisa.
Nikifuata kanuni hii, baadaye nilikuja kugundua kwamba katika ulimwengu huu mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyofikiria, nikatenda mambo mema mengi kwa watu, lakini watu haohao wakaja kunitendea mambo mabaya ambayo baadhi sitayasahau maishani mwangu hata kama nimekwishawasamehe.
Duniani ni mahali pabaya, hata kama wewe ni mtu mwema kiasi gani, elewa tu kuna mtu mahali fulani anakuchukia na pengine mtu huyo umeishi naye vizuri, umemtendea mema, unamwita ndugu au rafiki, lakini anapanga kukudhuru au kukuharibia mambo yako, huu ni ukweli ambao wanadamu inatupasa kuufahamu.
Nikaja kukutana na msemo wa siku nyingi usemao “Tenda wema uende zako usingoje shukurani” ambao uliponya maisha yangu na kunipunguzia maumivu niliyokuwa nikiyapata baada ya kutenda wema halafu nikalipwa ubaya! Baada ya hapo maisha yangu yamekuwa mepesi, bila maumivu kwa sababu sitarajii kulipwa wema na mtu ninayemtendea wema.
Watu wengi sana wameumizwa maishani mwao na ninafahamu wapo hata ambao walifikia hatua ya kukatisha maisha yao, baadhi hivi ninavyoandika wapo magerezani kwa sababu tu walitendewa ubaya na watu waliowatendea mema! Ndivyo maisha yalivyo, si lazima mtu uliyemtendea wema akulipe yeye, utalipwa na watu wengine mbele ya safari.
Hebu fikiria maumivu ya kumsomesha binti kutoka familia masikini mpaka chuo kikuu mkiwa mmekubaliana kwamba akimaliza shahada yake ya sheria atakuwa mke wako, ukajinyima kwa kula dagaa, kutembea kwa miguu, wadogo zako wakakosa elimu kwa sababu ya mwanamke huyu, lakini mwisho, akiwa amevaa joho siku ya mahafali yake pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anakuambia: “Hatuwezi kuoana, kwani wewe siyo ‘type’ yangu!” yaani siyo daraja lake, hujasoma, amekutana na msomi mwenzake.
Maumivu yake utakapofikiria jinsi ulivyowekeza kwa msichana huyo ni makali mno, usipoangalia unaweza kuanguka chini ukafa! Kwa nini? Kwa sababu ulitenda wema na ukasubiri kulipwa wema au shukrani. Hili ndilo kosa ambalo wanadamu wengi tunalifanya sana maishani, unatenda wema kwa mtu halafu unasubiri kulipwa.
Ukweli wa mambo ni kwamba mtu unayemtendea wema mara nyingi hatakulipa, bali utalipwa na watu wengine mbele ya safari kama ambavyo wewe ulisaidiwa na watu wengine wengi huko ulikotoka na hukuwalipa, lazima kuna mtu amewahi kukusaidia kitu fulani mahali fulani, hutamwona tena maishani, malipo yake ni wewe kumsaidia mtu aliyeko mbele yako bila kutarajia kulipwa fadhila.
Kama tutaishi kwa kanuni hii, hakika tutakuwa tumefuata kanuni ya Mungu ya mafanikio na hatutaishi kwa maumivu tena pale ambapo watu tuliowasaidia kufika mahali fulani maishani watatutukana mitandaoni au wataturushia tope kwenye magari yao wakati wanapita kwa sababu tu wamefanikiwa, hata uwe mjanja vipi lazima ukubali kutumika kama ngazi au karai wakati wa ujenzi wa ghorofa ambalo litakapokamilika ngazi na karai hutupwa kule, hivyo ndivyo maisha yalivyo.
Kuna mtu mahali fulani anasoma ukurasa huu, moyo wake umejawa na maumivu makali sana, ana chuki mno, sababu alitumia kila kitu alichokuwa nacho kuwasaidia watu wengine wafanikiwe, wakati mwingine akawasahau mpaka watoto wake wa kuzaa ili asomeshe ndugu zake, leo hii wamemkimbia, wamemtenga, wanamwona ni mjinga na wanamzomea!
Nataka nimtie moyo mtu huyu, mchango wako kwa familia yako hautapotea bure, Mungu wa mbinguni anauona, wakati wa kukulipa utakapofika atamtuma mtu si lazima wawe hao uliowasaidia na muujiza wako utatokea! Yawezekana usishuhudie kwa macho au haitatokea katika kipindi chako, lakini mahali fulani maishani mwanao, mjukuu wako atakuja kulipwa sababu ya wema ulioutenda wewe.
Mwanadamu hawezi kuukimbia wema au ubaya alioutenda, utamfuata popote atakapokuwa hata kama ni kaburini, huu ni ukweli, nimeishi kwa imani hii miaka mingi na ninayaona matunda yake maishani mwangu. Kama ulitenda wema malipo utayapata, kama ulitenda ubaya pia malipo utayapata.
Hivyo hakuna sababu ya kuumia sana, uchungu ulionao moyoni unakufunga miguu ya kusonga mbele, umegubika akili yako na kufanya ushindwe hata kuzioa fursa za maisha kwa sababu siku zote unawawaza tu waliokutendea ubaya na kubaki unatokwa na machozi kila unapokumbuka wema wako ambao mwisho wa siku umelipwa ubaya.
Katika kitabu changu kiitwacho SHERIA KUMI ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWENDA KWENYE MAFANIKIO, nimemtaja Mjapan mmoja aliyesaidia kubadilisha akili yangu, huyu alinikuta mtaani nikiuza karanga, akazinunua zote na baadaye akaniambia maneno “You are very intelligent” yaani “Una akili sana”, maneno ambayo sikuwahi kuambiwa shuleni au mitaani, siku zote niliitwa mjinga.
Maneno haya ya Mjapan ndiyo yaliyonifanya nibadilike, kwani tangu siku hiyo nilijiamini kupita kiasi, nikaona hakuna ambacho sikuwa na uwezo kukifanya hapa duniani, mfumo wa elimu ulinifanya nijione mjinga kwa sababu nilifeli kila somo, hii ni kwa sababu walimu wangu walitangulia kuniita mjinga, nikaamini nilikuwa mjinga hivyo nikawa ninafeli darasani, matokeo yake sikufaulu mtihani darasa la saba wala sikusoma sekondari.
Jina hili ‘MJINGA’ nililokuwa nikiitwa na watu lilinifunga miguu yangu, linaniibia uwezo wangu, hatimaye kwa muda mrefu nikawa fukara, bila Mjapan kuniambia “You are intelligent” kwa mara ya kwanza, hakika ningekuwa fukara mpaka leo, pengine nikinywa gongo kijijini kwetu! Habari ya kusikitisha kabisa!
Hasira ulizonazo moyoni mwako, kwa sababu ulijitoa sana kusaidia ndugu zako, kusomesha wasio na uwezo ambao baadaye walipofanikiwa walikuona mjinga kwa sababu hukusomesha watoto wako ukawasomesha wao, zinakufunga miguu na kukufanya usisonge mbele, nakuomba uwasamehe, achana nao, usilie tena!
Ukiyafanya haya utaona umekuwa mwepesi, akili yako imefunguka, macho yako yameanza kuziona fursa na maisha yako yatachipuka upya na Mungu atakulipa kwa wema ulioutenda ambao ninaamini kabisa anaukumbuka, acha kuendelea kutegemea uliowasaidia nao watakusaidia, uliowatendea mema, eti nao watakutendea mema, dunia haiko hivyo, utalipwa na watu wengine mbele ya safari.
Kukutia moyo hebu nikushirikishe ushuhuda huu ulionitokea mimi jana Novemba 24, 2017 ili upate kuamini kwamba Mungu hulipa wanaotenda wema na kwamba uliowasaidia siyo watakaokusaidia, bali Mungu atawatuma watu wafanyike malaika na kukuondoa kwenye tatizo ulilonalo.
Siku hizi maisha yangu yamekuwa; asubuhi kupeleka watoto shule, kupita kwa mama kumsalimia, kazini, saa kumi niende nyumbani kwa mama kumwona kisha ninyooshe chuoni ambako masomo huanza saa kumi na moja mpaka saa tatu au nne usiku, Jumapili kanisani au kwenye mwaliko mahali fulani kuzungumza na vijana.
Siku ninayoiongelea nilitoka darasani Chuo Kikuu cha Tumaini ambako ninasoma Shahada ya Mawasiliano ya Umma mwaka wa kwanza, saa 3:10, mke wangu alikuja pale kunichukua na kunipeleka moja kwa moja nyumbani kwa mama yangu ambaye kwa muda amekuwa dhaifu, wasomaji wa ukurasa huu wanaelewa kwa sababu nimewashirikisha sana juu ya ugonjwa wa mama yangu.
Nilikuta hali yake si njema sana, anaumwa! Shinikizo lake la damu lilikuwa limeshuka, hakika nikachanganyikiwa, uamuzi pekee niliouchukua ukawa ni kuita gari la wagonjwa ili tumuwahishe haraka Hospitali ya Aga-Khan, sikujali tena juu ya mgogoro ambao niliuanzisha na hospitali hiyo wiki chache zilizopita, nilichokihitaji ni matibabu ya mama yangu.
Gharama ya kulipigia gari la wagonjwa ilikuwa shilingi laki moja, mfukoni nilikuwa na laki moja na nusu tu! Tulipofika hospitali nikalipa wenye gari na kubakiwa na shilingi elfu hamsini, mgonjwa akapokelewa na kuanza kupewa matibabu kwenye kitengo cha dharura.
Hospitali ya Aga-Khan haipokei wagonjwa wa Bima ya Afya, jambo ambalo kwa muda mrefu nimekuwa nikilipigania mpaka Wizara ya Afya, hivyo kilichokuwa kikihitajika hapo ni fedha, ndugu yenu situmii kadi ya benki, ninaamini huwa zinanifanya na kuwa na matumizi mabaya! Tukaitana kando na mke wangu kujadili tufanye nini, kama familia tukafikia uamuzi wa kuagiza fedha mahali fulani.
Muda mfupi baadaye simu yangu ikaita, nilipopokea alikuwa ni rafiki yangu, Deo, hili siyo jina la kutunga, alikuwa mfanyakazi wa EWURA, anafahamika! Tukasalimiana nikamwambia mama yangu alikuwa mgonjwa na ndiyo tulikuwa tumefika Hospitali ya Aga-Khan.
“Niko Tegeta, nakuja hapo sasa hivi Eric, wewe ni rafiki yangu lazima nije nimwone mama!”
“Karibu sana.”
Tegeta na ilipo Hospitali ya Aga-Khan, ni umbali wa kama kilometa thelathini hivi, tayari ilishatimu saa tano usiku, lakini Deo aliondoka nyumbani kwake na kuendesha gari hadi Aga-Khan hospitalini, huu ni uungwana ambao sijawahi kuushuhudia siku za hivi karibuni, huu ndiyo unaitwa undugu, wanaotafsiri undugu kama kuzaliwa tumbo moja wanakosea sana.
Deo alifika, akamwona mama, cha kushangaza ambacho sikukitarajia wakati anaondoka alifungua pochi yake na kunikabidhi dola elfu moja mia saba! Kwa shilingi za Kitanzania ni kama shilingi milioni tatu na laki nane! Sitaki kuficha nilipatwa na mshtuko, sikutarajia, kitendo cha kuja tu kumwona mama yangu usiku ule kilitosha kabisa, lakini bado akaniongezea kiasi hicho cha fedha, tena katika wakati ambao ninahitaji mno kuwa na fedha. MUNGU AMBARIKI SANA DEO.
Ninachotaka kuonesha hapa ni kwamba, Mungu amemtuma mtu kuja kunilipa wema ambao nimewahi kuufanya mahali fulani huko nyuma kwa mtu ambaye pamoja na kumtendea wema alinitukana, alinidharau, aliniona mjinga! Hivi ndivyo ilivyo katika maisha, tusitegemee kulipwa na watu tuliowatendea mema, tutaumia kila siku na tutapatwa hata na magonjwa ya moyo na kufa.
Tuwasamehe wote waliotukosea kisha tumwachie Mungu ashughulike nao, tukumbuke tu kwamba Mungu anaukumbuka wema wetu, inapobidi kumkumbusha kama alivyofanya Ezekia, basi tugeukia ukuta na kulia mbele zake tukimwambia “Baba kumbuka wale niliowasomesha, kumbuka yule nilimwozesha, kumbuke yule nilimnunulia dawa…” tusiwakumbushe wale tuliowatendea wema na kuwaambia “Wewe nilikufanyia hivi na vile, leo unaringa?” Mwachie Mungu anaona, yeye si kipofu.
Mungu awabariki sana,
Ni mimi ndugu yenu,
Shigongo Eric James.

UPDATES: MAUAJI YA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA – MOSHI

Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha Pili katika Shule ya Scolastica, Edward Shayo (kushoto) akiwa na watuhumiwa wenzake wawili (waliofungwa pingu mikononi) wakipelekwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi jana.

Picha na Dionis Nyato wa Mwananchi Communications

%d bloggers like this: