Follow Elimu Leo Blog on WordPress.com

Member of The Internet Defense League

Sajili Barua pepe yako upate habari mpya kila zinapotokea

Join 1,637 other followers

Idadi ya waliotutembelea

  • 207,897

VIDEO: MZEE ALIYETENGENEZA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME NJOMBE

Bw. Pwagu mbunifu aliyeshia darasa la 7 na kutengeneza mtambo wa kuzalisha umeme na kuusambaza kijijini kwake huko Njombe. mtazame hapo chini anavyoelezea ubunifu wake huo.

 

Video kwa hisani ya BBC.

Advertisements

MIAKA 10 YA CHUO KIKUU CHA ARDHI: AFISA MIKOPO YA WANAFUNZI ATUMBULIWA KWA UZEMBE

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa kassim Majaliwa amekitaka Chuo Kikuu cha Ardhi nchini kuendelea kutekeleza mpango mkakati waliojiwekea ili kufikia malengo yanayo kusudiwa na Taifa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho ambapo amekitaka , Chuo hicho kuwa na kamapuni itakayosimamia ujenzi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na siyo jina la Chuo kutumika vibaya na kuratibu sifa ya Chuo.

Waziri Majaliwa amesema Chuo hicho kimekuwa kikiisaidia serikali kujenga majengo yenye viwango kwa garama nafuu, hivyo amezitaka taasisi za serikali kukitumia Chuo hicho katika ujenzi wa majengo mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Chuo kikuu cha Ardhi kimekuwa kikifanya vizuri katika ujenzi, usanifu wa majengo na kwa kutambua kazi ya Chuo hicho tayari Wizara imetoa zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya Ualimu, na shule.

Baada ya kukamilika kwa mkutano huo, Waziri Ndalichako alikutana na wanafunzi wa Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza changamoto mbalimbali ambapo wanafunzi walimweleza Waziri kuwa hadi sasa hawajaingiziwa mikopo yao kwa kile kilichoelezwa kuwa wanafunzi bado hawajafungua Akaunti, na ndiyo Wizara alipohitaji maelezo kutoka kwa Afisa mikopo majibu ambayo waziri hakuridhika nayo na ndiyo alipoomba maelezo.

Hata hivyo kutokana na maelezo ambayo hakuridhika nayo,Waziri aliamua kuondolewa mara moja kwa afisa mikopo katika Chuo hicho.

UONGOZI WA SHULE YA SCOLASTICA WAHUSISHWA NA KIFO CHA MWANAFUNZI WAO

Marehemu Humphrey Jackson Makundi enzi za uhai wake

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah amethibitisha kwamba tarehe 10 November 2017 walipata taarifa rasmi kuhusu kifo cha utatanishi cha mtoto ambae ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo, Moshi – Kilimanjaro.

Kamanda Issah amesema walifanya mahojiano wakianzia na mmiliki wa shule hiyo, walinzi, majirani na baadhi ya wanafunzi ambapo walilazimika kuwazuia baadhi ya watu ili kuendelea na uchunguzi.

Kamanda Issah alisema familia ya mtoto ambae alipotea ilikuja na plan B ambayo ililisaidia jeshi la polisi baada ya kusema mtoto wao tayari ameshafariki na wakihusisha kifo hicho moja kwa moja na mmiliki wa shule.

Kwa mjibu wa baba mdogo wa marehemu aliyetambulika kwa jina moja la Makundi, amesema wao kama familia walipata taarifa ya mtoto kupotea tarehe 7 japo hakuwa wanajua alipotea lini. Walivyopata taarifa wakafunga safari kutoka Dodoma kuja kufatilia na kwenda shuleni ambako anasema walipata taarifa zisizoridhisha kutokana na mazingira waliyoyakuta.

Wakati wanafatilia kwa kushirikiana na shule na watu wengine na kituo cha Polisi cha Himo, wakapata taarifa kwamba kuna mwili uliokotwa mtoni karibia na shule hiyo ya Scolastica na tayari ulikwishazikwa. Hata hivyo baada ya kufukuliwa mwili huo ulibainika kuwa ni wa mwanafunzi huyo aliyeripotiwa kupotea.

Taarifa zaidi zinasema uongozi wa shule hiyo unahusishwa kuhika na tukio hilo kutokana na ukweli kwamba wanafamilia walipofika shuleni hapo hawakukuta kitu chochote ambacho ni mali ya marehemu kama vile madaftari, nguo, na vifaa vingine alivyokuwa akivitumia shuleni hapo. Hata hivyo wananchi wa eneo hilo walisikika kuushutumu uongozi wa shule hiyo kwa tabia yao ya kuendekeza vitendo vya kikatiri dhidi ya wanafunzi wao.

Polisi mkoani Kilimanjaro bado inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na inamshikilia Mkuu wa shule hiyo.

CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA ELIMU

Jamhuri ya Watu wa China imesema itaendela kuisaidia Tanzania katika sekta ya Elimu kwenye eneo la Elimu ya Juu, utoaji wa mafunzo ya Ufundi pamoja na kusaidia garama za uchapishaji wa vitabu vya masomo ya Sayansi kwa ajili ya shule za msingi na Sekondari.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China nchini Tanzania Wang Ke wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ofisi ndogo zilizopo jijini Dar es Saalam.

Katika mazungumzo yao Waziri Ndalichako amesema garama za uchapaji wa Vitabu ni kubwa hivyo ni vyema Wizara ikawa na mitambo yake ya kuchapia vitabu ambayo itakuwa endelevu suala ambalo Balozi Wang Ke amekubaliana nalo na kuitaka Wizara kuandaa maombi ya mashine hiyo ili ubalozi uweze kufanyia kazi.

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO AWAMU YA TATU 2017

TAARIFA KWA UMMA
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano Awamu ya Tatu
mwaka 2017 wataanza masomo yao tarehe 21 Novemba, 2017 na
hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote
wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo
mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 4 Desemba 2017 ambayo
ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi.
Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya Ofisi ya RaisTAMISEMI
kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, inabidi
ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano
Awamu ya Tatu mwaka mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule
(joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya RaisTAMISEMI
ya http://www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais -TAMISEMI

Kuona majina bofya <HAPA>

Kupakua fomu ya kujiunga bofya <HAPA>

%d bloggers like this: