Home » Articles posted by Elimu Leo

Author Archives: Elimu Leo

BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ELIMU PROF. NDALICHAKO

Habari za muda huu mama, matumaini yangu ni kuwa u mzima wa afya.
Leo hii nimeamua kuchukua nafasi hii kukuandikia barua hii ya wazi kutokana na kuguswa na hali ilivyo katika sekta ya elimu nchini.

Kwa miaka mingi elimu yetu imekuwa ikipitia katika historia ndefu ambapo katika historia hiyo ina wingi wa mafanikio na wingi wa changamoto ndani yake. Aidha, tumepita katika nyakati tofauti tofauti zinazoeleweka na zisizoeleweka kimtazamo, kifalsafa na kisera. Kimsingi, bado tuna wingi wa changamoto katika mfumo wetu wa elimu.

Ili elimu yetu iwe na tija na mantiki kwa Watanzania kufikia nchi ya viwanda sharti ilingane na iendane na mahitaji yetu kwa wakati husika. Yote haya yatafanikiwa kwa kuhakikisha kuwa tunazitatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza kabla ya kuwa kubwa na kugeuka kuwa matatizo hivyo kushindwa kutatuliwa.

Kwa kipindi kirefu sasa changamoto za mimba kwa wanafunzi, utoro uliokithiri kwa wanafunzi, upungufu na uchakavu wa miundombinu ya shule kama vile vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, matundu ya vyoo, ofisi za walimu, maabara na hosteli pamoja na Uhaba wa walimu zimekuwa zikisababisha elimu yetu kuzidi kudhorota siku hadi siku na hivyo kuturudisha nyuma kufikia malengo tuliyoyakusudia. Katika kipindi cha mwaka 2015-2017 changamoto hizi zimezidi kuwa kubwa kuliko miaka ya nyuma. Lakini kwa miaka ya hivi karibuni, shule za binafsi zimezidi kung’ara katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya elimu ya msingi na sekondari, hii yote ilitokana na ubidhaishaji wa elimu ambao kwa kiasi kikubwa umeendeleza wimbi la matabaka kwa shule za watoto wa wenye nacho (shule binafsi) kuzidi kufanya vizuri huku shule za watoto wa wasio nacho (shule za umma) kuzidi kuvurunda.

Aidha, naipongeza wizara yako na serikali kwa ujumla kwa mapenzi yenu mema kwa Watanzania kwa kuona mbali na kuja na wazo chanya na mbadala kwa hili na hivyo kuifanya elimu kupatikana bure kwa shule za umma lengo likiwa ni kuwawezesha watoto wa walalahoi kupata elimu bila kukumbwa na kikwazo chochote cha gharama kama ambavyo serikali iliweza kujinasibu kupitia tamko la sera kipengele cha 3.3.2 kuwa itahakikisha inaondoa vikwazo vyote vinavyopelekea mwanafunzi kushindwa kukamilisha mzunguko wake wa kielimu. Pamoja na jitihada zote hizi, matabaka katika utoaji wa elimu bado yapo na yataendelea kuwapo mpaka pale mtakapoamua kuweka uwiano sawa wa utoaji elimu kwa shule zote (za umma na binafsi).

Aghalabu, Sera hii ni njema sana na inafaa kupigiwa chapuo na kila mwenye mapenzi mema na walalahoi. Mbali na uzuri na mapenzi mema ya sera hii kwa watoto wa walalahoi, sera hii pia imekuwa mzigo kwa watekelezaji wake kwani wengi wa watanzania hawaelewi hasa mipaka katika utekelezaji wake na hivyo kupelekea kuwaachia mzigo wote walimu huku wakiamini kuwa serikali inalipia kila kitu katika kutoa huduma ya elimu kwa watoto wao hivyo hata michango ya kimaendeleo inapoletwa na walimu hukataa kutoa ushirikiano kwao kwa kigezo kuwa serikali iliahidi kuitoa huduma ya elimu bure na hivyo ninyi mnaotuambia tuchangia mchango kwaajili ya kitu Fulani mnataka kutuibia.

Sambamba na hapo, hivi majuzi tumesikia mkisema kuwa haruhusiwi mwalimu yeyote kuchangisha fedha kwaajili ya mchango wowote. Hapa hatujawaelewa kabisa, Madhara ya tamko hili ni kubwa kuliko faida zake na kupitia tamko hili mnakwenda kuizika elimu ya nchi hii kwa upande wa shule za umma waziwazi. Ni kwa kupitia tamko hili watoto hawataweza kula chakula cha mchana, kufanya majaribio ya wiki, mwezi na hata robo muhula ilhali mazoezi haya ndiyo yalikuwa msaada mkubwa sana kwao katika kunyanyua ufaulu wao kitaaluma. Aidha, ni kwa kupitia tamko hili, shule za umma zitazidi kushika mkia kuliko kipindi chochote kile. Vilevile, shule nyingi zitashindwa kuendeleza huduma nyingi za msingi na za maendeleo kitaaluma kwa wanafunzi na shule ambazo zilikuwa zinatokana na changizo za wazazi kama vile, changizo kwaajili ya kupata walimu wa ziada kwa shule za msingi na walimu wa masomo ya sayansi kwa shule za sekondari. Hivyo basi ninaomba muandae mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo kama kweli mna mapenzi mema na elimu yetu nchini.

Mathalani, ili kuhakikisha kuwa elimu hii inayotolewa ambayo tumekusudia imfikie kila Mtanzania inakuwa bora na yenye manufaa kwa watanzania wote sharti tuhakikishe kuwa tunakuwa na watekelezaji wa kutosha. Ni dhahiri kuwa nchi yetu kwasasa inakumbwa na uhaba mkubwa sana wa walimu. Kulingana na maelezo aliyoyatoa aliekuwa Naibu Katibu Mkuu CWT Ndg. Ezekiel Oluoch wakat akihojiwa na gazeti la Rai la January 2017, alisema kuwa kwa upande wa shule za msingi kuna uhitaji wa walimu 300,000 ili kukidhi haja huku akiainisha wazi kuwa walimu waliopo kwa wakati huo wakiwa ni 200,000 hivyo kwa upande wa shule za msingi kuna uhabai wa walimu 100,000 kufikia Januari 2017. Vivyo hivyo kwa upande wa sekondari aliainisha kuwa kuna uhitaji wa walimu 135,000 ili kukidhi haja huku walimu waliopo wakiwa ni 85,000 hali inayosababisha kuwa na uhitaji wa walimu 50,000. Pia, aliainisha kuwa hakuna walimu wa kutosha wa masomo ya Uraia, Lugha (Kingereza), Fizikia, Biolojia na Kemia.

Kulingana na maelezo yake, aliainisha kuwa moja ya sababu kubwa zinazopelekea uhaba huu kuzidi kukua ni pamoja na wimbi la wastaafu kuzidi kuongezeka kila mwaka. Mnamo Januari 2018 serikali iliweza kuajiri walimu 3,033 wa sekondari na shule za msingi. Katika idadi hiyo, walimu 266 (sekondari) na 2,067 (shule za msingi). Hii ni mwaka mmoja baada ya Mwl. Oluoch kuainisha hali halisi ya walimu nchini sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa ndani ya huo mwaka ni walimu wangapi wamestaafu? Au ni walimu wangapi walikuwa na vyeti feki na hivyo kuondolewa kazini?

Binafsi nimefanikiwa kuzitembelea shule kadhaa zilizopo wilaya ya Mwanga, Moshi Vijijini na Moshi Mjini. Kati ya shule zote nilizozitembelea (takribani shule 50 za msingi na 15 za sekondari), nyingi za msingi zina walimu 4, 3, 2 na nyingine nimekuta mwalimu mmoja. Kwa uhalisia walimu watatu hawawezi kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora zaidi sana watakuwa wakifanya mambo bora liende kutokana na rundikano la majukumu kwao. Kwa hali ilivyo sasa, darasa la awali linatakiwa kuwa na mwalimu wake ambae hatahusika na darasa linguine tofauti na hilo, hali kadhalika kwa darasa la kwanza na la pili. Kwa misingi hiyo kwa shule yenye walimu watatu atabakia mwalimu mmoja tu ambae ndie atahusika kufundisha kuanzia darasa la 3-7.

Kwa upande wa shule za sekondari, kuna shida kubwa ya walimu wa masomo ya sayansi, mathalani; Fizikia, Hesabu, Kemia na Biolojia. Shule nyingi nilizofika katika mkoa huu wa Kilimanjaro hii sio changamoto tena bali ni tatizo. Shule nyingi unakuta zina walimu wawili au mmoja wa masomo haya. Kuna shule hakuna kabisa walimu wa masomo haya na hivyo wanafunzi hujisomea wenyewe pasi na kufundishwa na mwalimu huku wakisubiri mitihani ya kitaifa.

Dhumuni la barua hii hasa ni kukuomba kufungulia milango kwa Wizara yako kuzikumbuka shule hizi kwa kuongeza walimu nchini na kuzifanyia kazi changamoto nyingine nilizozitaja ili kufikia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2024/25 katika kuhakikisha tunakuwa nchi yenye uchumi wa kati wa viwanda (Industrialized Country).
Aidha, Tanzania tutaweza kufikia adhma hii kwa kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kufanya tendo la uhawilishaji wa maarifa kutokuwa mzigo kwa wanafunzi na walimu na hivyo kuwafanya kulifurahia.

Tulikazana kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na maabara lakini vema tukatambua kuwa kuwa na maabara bila ya kuwa na walimu wa kutosha wenye weledi wa kutosha kwenye masomo yanaendana na uwapo wa maabar hakutaweza kuwafanya wanafunzi kuvutiwa na maabara hizo. Elimu bila malipo haitafanikiwa kwa kiwango tulichokusudia kama hakutakuwa na walimu wa kutosha watakaosaidia katika kuitekeleza adhma nzuri ya serikali. Wizi wa mitihani hautakoma kama tutakuwa tukiendelea kuwahimiza walimu wafaulishe ilhali walimu wa kufundisha hawakidhi haja, tutakuwa tunajidanganya tu. Huwa najiuliza inakuwaje shule yenye mwalimu mmoja au yenye walimu watatu inafaulisha watoto wote ama wanafunzi nane kati ya 38 kufeli kama sio kudanganyana?

Nakuomba kupitia wizara yako kuliangalia hili kwa mapana yake. Wakati tunapigania kila Mtanzania kupata elimu ni vema kuhakikisha elimu anayoipata ni bora na wale wanaohusika kuitekeleza elimu hii (walimu) hawaumii na kuvunjika moyo.
Kabla ya kuanza na viwanda ni vema tukaanza na mapinduzi ya elimu yetu ili kuzalisha wataalamu wa ndani watakaosaidia katika viwanda hivyo.

Mwisho, utekelezaji wa elimu bila malipo uendane na maandalizi ya kuhakikisha wanafunzi wanaopata nafasi ya kujiunga na vyuo vya kati au vyuo vikuu nchini wanakamilisha mzunguko wa elimu yao bila kikwazo chochote kama ambavyo serikali ilivyojidhatiti kupitia sera ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 2014 kuwa itahakikisha kuwa wanafunzi wanakamilisha mzunguko wao wa kielimu bila vikwazo vyovyote. Sipendekezi utoaji wa mikopo kwa wanafunzi hao bali napendekeza utolewaji wa elimu kwa wanafunzi hao kufanyika bure bila malipo ama malipo hayo kuwa ya bei nafuu ambayo watanzania wa namna na vipato vya nchini wataweza kumudu gharama hizo.

Nashukuru kwa kuchukua muda wako kusoma waraka huu na ni matarajio yangu kuwa utaufanyia kazi. Nakutakia utekelezaji mwema.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Ndimi,
Gibson Johnson Eliaform Mdakama
0766 548 471/ 0676 108 126
mdakamadegibson112@gmail.com

Advertisements

HABARI NJEMA KUTOKA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP)

Image result for tsnp logo

Tanzania Students Networking Program is happy to announce to all Secondary, diploma and ongoing university students that, on 22- January 2018; TSNP signed an agreement of co-operation with Mr. Samuel Chatelle, study overseas agent from China through its International Relations and External Relations Department (IAER). This co-operation is expected to open doors for all Eligible Tanzanian Students to further their Higher Level Education in China at all levels, both graduates and undergraduates; as well as foundation courses.

GoldKitty is a Chinese agent with links to more than 50 Chinese Universities and Colleges; with more than 100 Course offerings for you to choose from, making sure you study what you love!

With this form, you are welcome to express an interest to study in China by responding to few prompts. TSNP will then communicate with the agent and verify on the possibility of getting a full or partial scholarship on your field of study.

In as much as we strongly recommend Tanzanian students to take advantage of this opportunity; we notify the public that TSNP only stands as a middleman to protect the interests of both the students and the agent. Due to this, eligible students may be required to incur both DHL and Agents fees as per an agreeable negotiation between the student and agent; for every scholarship secured.

After filling this form, The director of Foreign Affairs and International relations will get back to you within 5 hours or less, it is strongly advised that you provide an active email address

Tuma maombi yako hapa >>>>https://docs.google.com/forms/d/1sbxjxqv2sewa7pxJ6aBvs99FJ4tzGMCo1660CCxK4e8/viewform?edit_requested=true

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

*Moses E Katala,*
Director of Foreign Affairs and International Relations, TSNP*
tsnp.students@yahoo.com

 

AGIZO LA NDALICHAKO KWA TBA KUHUSU CHUO KIKUU CHA MLOGANZILA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameipa wiki moja  Wakala wa Majengo nchin- TBA- Kuhakikisha ujenzi wa majengo mbalimbali  unaanza mara moja ikiwa ni pamoja na kuongeza mafundi pamoja na kupeleka vifaa vya ujenzi katika Mradi wa  Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila.
Prof.  Ndalichako ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa, hosteli, ofisi na bwalo la Chakula katika Chuo Kikuu hicho kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo amesema hajaridhishwa na kasi ujenzi huo.
Waziri Ndalichako amesema Wizara tayari ilishaipatia TBA kiasi cha shilingi bilioni 3.9 kama malipo ya awali lakini mpaka sasa hakuna jengo lolote ambalo limeshaanza kujengwa na wala hakuna vifaa vya ujenzi katika eneo hilo zaidi ya kuchimbwa misingi tu.
Waziri Ndalichako amesema hatavumilia kuona udahili wa  wanafunzi wa fani za Afya unachelewa katika kampasi hiyo kwa kuwa  lengo la serikali ni kuongeza idadi ya wanafunzi wa fani hizo nchini.
Naye Kaimu Meneja wa Mkoa kutoka TBA Manase Kalage amemwakikisha Waziri kuwa maagizo aliyoyatoa watayatekeleza ikiwa ni pamoja na kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA
20/01/2018

FAHAMU ALICHOKIFANYA FLAVIANA MATATA KWENYE ELIMU HUKO BAGAMOYO

Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata amekabidhi jengo la madarasa mawili yatakayotumika na darasa la sita na la saba pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule katika Shule ya Msingi Msinune iliyopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

Flaviana ameeleza kuwa lengo kuu la kujenga jengo hilo ni kusaidia jitihada za kuinua elimu nchini kwa kuboresha miundombinu ya kusomea.

Mwanamitindo huyu alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa kijiji hicho cha Msinune mwaka 2014 ambao walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na kumalizia ujenzi wa madarasa.

Flaviana amenukuliwa akisema;

“Sisi kama vijana wa Tanzania tunalo jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake.” 

 

UDHAMINI WA MASOMO CHUO KIKUU CHA ARDHI 2018/19

 

Ardhi University

Bofya viunganishi vifuatavyo

Tangazo la udhamini

Taarifa za udhamini

Fomu ya maombi

 

%d bloggers like this: