Home » Matangazo » NAFASI ZA MASOMO CHUO CHA MADINI KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA 2017/18

NAFASI ZA MASOMO CHUO CHA MADINI KWA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA 2017/18

Advertisements

 

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO KATIKA NGAZI YA
ASTASHAHADA/STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Chuo cha Madini Dodoma kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini, kina uzoefu wa zaidi ya miaka thelathini (30) katika kufundisha wataalamu wa ngazi ya kati katika sekta ya madini. Tangu mwaka 2012, Chuo cha Madini kilianza pia kutoa mafunzo katika sekta za Mafuta, Gesi na Mazingira.
Chuo kimepewa ithibati kamili na Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) kutoa mafunzo katika ngazi ya Astashahada hadi Stashahada (NTA level 4 – 6) katika mfumo wa umahili (CBET) tangu tarehe 27/4/2007.
Chuo kinakaribisha maombi kwa waombaji wenye sifa kuomba kusoma Astashahada/Stashahada kwa kozi zifuatazo:
 Jiolojia na Utafutaji Madini (Geology and Mineral Exploration)
 Uhandisi Migodi (Mining Engineering)
 Uhandisi Uchenjuaji Madini (Mineral Processing Engineering)
 Sayansi ya Mafuta na Gesi (Petroleum Geosciences )
 Uhandisi na Usimamizi wa Mazingira Migodini (Environmental Engineering and Management in Mines)
Hakutakuwa na ufadhili kwa waombaji watakaochaguliwa katika kozi zote
SIFA ZA KUJIUNGA
 Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form IV) na awe amefaulu masomo ya Fizikia, Kemia, Hisabati na masomo mengine mawili (2) kwa kiwango cha kuanzia D; au
 Awe na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari pamoja na Cheti cha VETA ngazi ya ufundi sadifu katika fani za Uhandisi Umeme, Mitambo au Ujenzi.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wote wenye sifa wanatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuituma Chuoni moja kwa moja. Fomu za maombi zinapatikana Chuoni, Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi za Madini zilizopo Mbeya, Tabora, Mwanza, Kahama, Dar es Salaam, Musoma, Songea, Arusha, Tanga, Tunduru, Dodoma, Morogoro, Handeni, Merelani, Mpanda, Bukoba, Mtwara, Shinyanga, Chunya, Moshi, Nachingwea, Geita, Bariadi, Singida na Kigoma, au katika tovuti ya chuo: http://www.mri.ac.tz

Kwa maelezo/msaada zaidi wasiliana nasi kupitia:

0784 893 116 / 0764 910 385 / 0717 361 771 / 0753 858 028
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 20/8/ 2017 saa 9:30 alasiri.
Tarehe ya kuanza masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ni 18/9/2017.
NB:
 Maombi yote yatumwe Chuoni ndani ya muda uliopangwa
 Fomu za maombi ziambatanishwe na nakala halisi ya hati ya malipo ya benki (Pay-in Slip) yenye kiasi cha Tshs. 20,000/= na ilipwe kwenye akaunti ya Chuo

(Akaunti Na. 01J1082316900, CRDB, CHUO CHA MADINI DODOMA).
Fomu za maombi zitumwe kwa:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Madini Dodoma,
S. L. P 1696,
Dodoma

Pakua fomu ya maombi hapa >>>>MRI-Application-form-2017-2018-INTAKE

Advertisements

4 Comments

 1. David marwa says:

  Am David from masumbwe i want to join that school but i do take my study from kenya what should i do to full fill

  Like

 2. Naitwa Sadik ningependa kufah kwa wale walio maliza Astashahada kwenye vyuo vingne za madini wanaruhusiwa kujiunga na stashada kwenye chuo chenu ?

  Like

 3. micky says:

  Naitwa micky nina phy D, Chem D, biology C, geography D, history D, civic D, English D, kiswahil D, math F ninaweza kujiunga na chuo chenu upande wa mining engineering

  Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: