Home » Habari » SHULE ZA MSINGI KENYA ZAANZA KUFUNDISHA KI-DIJITALI

SHULE ZA MSINGI KENYA ZAANZA KUFUNDISHA KI-DIJITALI

Advertisements

 

 

 

Zaidi ya shule 17,000 nchini kenya zimepokea vifaa (Laptop) vya kufundishia na kujifunza kwa njia ya ki-dijitali. Mtaala mpya wa elimu nchini humo unaelekeza kutumika kwa vifaa hivyo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili nchini kote na hadi sasa kiasi cha laptop 992,073 zimesambazwa katika shule 17,000 na zaidi ya walimu 95,000 wamepokea mafunzo ya kutumia mfumo huo mpya wa kufundishia.

Sanjali na hatua hizo, viwanda viwili vya kuunganisha vifaa hivyo vimejengwa katika vyuo vikuu vya Jomo Kenyatta na  Moi ili kuharakisha uzalishaji wa vifaa hivyo  vitakavyosambazwa kwenye shule zote za msingi za umma zipatazo 23,951 na kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kukabiliana na ushindani wa kimataifa katika umri mdogo.

Rais Uhuru Kenyetta na Makamu wake, William Rutto wamekagua maendeleo ya mpango huo wa serikali walipotembelea shule ya msingi Kathithyamaa wakati wa kampeni za urais zilizofanyika katika eneo la Machakosi hapo jana Jumanne.

“Tutaendelea kuunga mkono mpango huu wa kujifunza ki-dijitali hadi uzifikie shule zote za umma 23,951. Maudhui ya ki-dijitali yameshaandaliwa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili na wanafunzi hao sasa wanaweza kuyapata kupitia vifaa hivi,” alisema Rais Kenyetta.

Alisema pia shule zote za umma zinaunganishwa na mkongo wa taifa ili kuhakikisha upatikanaji wa mtandao utakaowezesha ukamilifu wa mpango huo. Rais Kenyatta amesema kwa Machakosi pekee, vifaa 25,731 vimesambazwa katika shule 609 kati ya shule 829 zenye miundombinu ya mpango huo ambapo jumla ya Shilingi za kenya Milioni 49.7 zimetumika.

Aidha, Rais Kenyetta ameahidi utoaji wa elimu bure kwa shule za sekondari kuanzia mwaka ujao ikiwa wakenya watamchagua kwa muhula wa pili wa urais.

 

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: