Home » 2017 » July

Monthly Archives: July 2017

Advertisements

ADA MPYA YA MAOMBI YA UDAHILI KWA VYUO VYA UMMA 2017/18

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ADA YA MAOMBI YA UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza linapenda kuvitaarifu Vyuo na Taasisi za Umma zinazotoa mafunzo yanayosimamiwa na Baraza (NACTE) pamoja na Umma kwa ujumla kuwa, Serikali imeagiza kuwa Ada ya Maombi ya Udahili (Admission Fee) inayotakiwa kutozwa kwa mwanafunzi anayeomba Udahili katika Vyuo/Taasisi za umma kwa mwaka wa masomo 2017/2018 isizidi shilingi Elfu Kumi (Tsh. 10,000/=) kuanzia sasa.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 28/07/2017

Advertisements

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI IMEBORESHA MFUMO WA UOMBAJI MIKOPO MTANDAONI

Wakuu na maafisa wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  wapo katika maandalizi ya mwisho ya kufanyia majaribio mfumo wake ulioboreshwa wa uombaji mikopo kupitia  olas.heslb.go.tz kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

OLAMS

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA Bw. Muze Ninkhambazi ambaye ameongoza mafunzo ya kuwapitisha idara na vitengo hivyo ili kuufahamu na kupata mapendekezo kutoka kwao kwa ajili ya kuboresha mambo muhimu yanayoingia katika mfumo huo kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Bw. Ninkhambazi amesema mabadiliko ya mfumo yanalenga kuufanya uwe wa kisasa zaidi na kuwarahisishia waombaji mikopo jinsi ya kuwasilisha taarifa zao Bodi. Aidha ameongeza kuwa maandalizi hayo yamewezesha kupata mchango mkubwa kutoka wa washiriki.

Miongoni mwa mabadiliko katika OLAMS ni pamoja na jinsi ya kufanya malipo, kuwasilisha viambatanisho muhimu kama cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne na saini za mwombaji na mdhamini wake.
Bodi ya Mikopo iliingia katika mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao mwaka wa masomo 2010/2011 na tangu wakati huo mfumo huo umekuwa ukiboreshwa ili kuendana na teknolojia mpya.

TAHADHALI KUTOKA CHUO KIKUU DAR (UDSM) KUHUSU TARATIBU ZA UDAHILI

Tumepata taarifa kwamba kuna matapeli wamekuwa wakiwahadaa wanafunzi wanaoomba udahili wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuwapa taratibu zisizo sahihi na kisha kuwaibia fedha zao.

Tunaomba kuujulisha umma kwa ujumla kwamba udahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unafanywa kwa kupitia mfumo wa kompyuta katika mtandao maalumu unaopatikana katika tovuti iliyopo kwenye anuani: udsm.admission.ac.tz. Maelezo ya jinsi ya kuomba udahili pamoja na habari nyingine za udahili zinapatikana katika tovuti ya chuo yenye anuani: www.udsm.ac.tz.

Maombi hayapokelewi kwa kujaza fomu. Pili, ada ya maombi ya udahili ni Shilingi 20,000/= tu ambazo zinalipwa kwa kutumia mitandao ya simu kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa kwenye mfumo wa udahili.

Tunatoa pole kwa waliopata usumbufu na tunasisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizo rasmi katika zoezi zima la udahili.

Tunawatakia udahili mwema.

Imetolewa na Kurugenzi ya Shahada za Awali

Simu:       0222410069 AU 0222410751

ORODHA YA VYUO NA PROGRAM ZILIZOZUILIWA NA TCU KUDAHILI WANAFUNZI KWA MWAKA 2017/18

TAARIFA KWA UMMA
VYUO NA PROGRAMU ZILIVYOZUILIWA KUDAHILI
WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA KWA MWAKA
WA MASOMO 2017/18

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kuuarifu umma kuwa,
mwezi Septemba na Oktoba mwaka 2016 ilifanya uhakiki wa vyuo vyote
vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni.
Ripoti ya uhakiki ilionesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo. Kwa
sababu hiyo, Tume imesitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa
kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo vifuatavyo:

1. Eckenforde Tanga University

2. Jomo Kenyatta University, Arusha

3. Kenyatta University, Arusha

4. United African University of Tanzania

5. International Medical and Technological University (IMTU)

6. University of Bagamoyo

7. St. Francis University College of Health and Allied Sciences

8. Archibishop James University College

9. Archibishop Mihayo University College

10.Cardinal Rugambwa Memorial University College

11.Kampala International University Dsm College

12.Marian University College

13.St. Johns University of Tanzania Msalato Centre

14.St. Johns University of Tanzania, Marks Centre

15.St. Joseph University College of Engineering and Technology

16.Teofilo Kisanji University

17.Teofilo Kisanji University Tabora Centre

18.Tumaini University, Mbeya Centre

19.Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)

Aidha, kutokana na mapungufu katika vyuo mbalimbali imeamriwa
kwamba jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa
kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo
2017/18. Kuona Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa
mwaka wa masomo 2017/18 tafadhali bonyeza hapa.

Aidha Tume inapenda kusisitiza kwamba, uamuzi huu hautawahusu
wanafunzi wanaondelea na masomo katika programu na vyuo husika.

Imetolewa na:
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
24 Julai 201

TAARIFA KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOTAKA KUSOMA CHETI AU DIPLOMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA CHETI AU STASHAHADA  KATIKA VYUO VINAVYOSIMAMIWA NA BARAZA  KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza linapenda kuwataarifu wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwezi Mei, 2017 na umma kwa ujumla; kuwa sasa wanaweza kutuma maombi  ya Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika Vyuo vya Serikali  kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya Udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.


Kwa wale ambao walishatuma maombi na wanataka kuongeza sifa ya kidato cha sita wanaweza kufanya hivyo sasa kupitia kurasa zao binafisi (Profile).Pia baraza linapenda kuwakumbusha na kuwahimiza wote wenye sifa kama zilivyo ainishwa kwenye kitabu cha Muongozo wa Udahili (Admission Guidebook) kinachopatikana kwenye tovuti ya Baraza kuwa, wafanye maombi yao mapema kabla ya tarehe 20 Agosti, 2017 kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sababu hakutakuwa na muda wa nyongeza.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 22/07/2017

%d bloggers like this: