Elimu Leo

Home » Fursa » NAFASI ZA MASOMO VYUO VYA MIFUGO 2017/18

NAFASI ZA MASOMO VYUO VYA MIFUGO 2017/18

TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY – LITA) KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18

1. Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kupitia Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo.
2. Katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake nane; Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina huduma ya malazi hivyo, watakaojiunga itabidi wajitegemee. Pia katika Kampasi zetu wanachuo wa ufadhili binafsi watakaopenda kukaa nje ya Kampasi wanaruhusiwa.
3. Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha nne wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada (Cheti). Pia vijana waliomaliza Kidato cha sita na wale wenye Astashahada (Cheti) katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba wanakaribishwa kwa ajili ya kujiunga na mafunzo kwa ngazi ya Stashahada (Diploma).

4. Kozi zinazotolewa ni kama ifuatavyo :
i) Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Certificate in Animal Health and Production – CAHP)
ii) Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Health and Production DAHP)
iii) Astashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara ya Veterinari (Certificate in Veterinary Laboratory          Technology – CVLT)
iv) Stashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara ya Veterinari (Diploma in Veterinary Laboratory Technology – DVLT)
v) Stashahada ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo (Diploma in Range Management and Tsetse Control-DRMTC)
5. Kampasi zinazotoa mafunzo hayo ni kama zinavyoonekana hapa chini na Kozi zitolewazo kwa kila Kampasi:
i) TENGERU S.L.P 3101 Arusha 0625874298 or 0727267335 DAHP & CAHP (Bweni na kutwa)
ii) MPWAPWA S.L.P 51 Mpwapwa 0629635700 or 0627627519 DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
iii) MOROGORO S.L.P 603 Morogoro 0752719458 or 0627885747 DAHP & CAHP (Bweni na kutwa)
iv) BUHURI S.L.P 1483 Tanga 0757954229 or 0785271732 DAHP CAHP (Bweni na kutwa)
v) MADABA S.L.P 568 Songea 0784641501 or 0629102761 DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
vi) TEMEKE S.L.P 39866 DSM 0754768877 or 0627627670 CVLT & DVLT (Kutwa)
vii) MABUKI S.L.P 115 Misungwi 0712581367 or 0623984122 CAHP (Bweni na kutwa)
viii) KIKULULA S.L.P 472 Karagwe 0763665322 or 0627627524 CAHP (Bweni na Kutwa)
ix) LITA HQ S.L.P 9152 DSM 0627629505

6. Sifa za mwombaji
i. Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Health and Production
DAHP)
Awe amemaliza elimu ya Kidato cha Sita na kufaulu masomo mawili ya Sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jiografia na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha Principal pass moja na subsidiary moja kwenye masomo ya sayansi.

AU
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC), CAHP NTA level 5, Agrovet

AU
Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP) waliosoma kwa mfumo wa muhula (term system)

ii. Stashahada ya Uendelezaji wa Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo (Diploma in Range Management and Tsetse Control-DRMTC)
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC- Term system) & CAHP NTA level 5, Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP)

iii. Stashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara ya Veterinari (Diploma in Veterinary Laboratory Technology DVLT)
Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Veterinary Laboratory technology (CVLT) NTA level 5

iv. Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Certificate in Animal Health and Production – CAHP) na Astashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara ya Veterinari (Certificate in Veterinary Laboratory Technology – CVLT)
Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo mawili ya sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jografia na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha alama ya D kwenye masomo manne,(mawili ya sayansi na mawili kwenye masomo mengine isipokuwa Dini na Upishi.
AU
Awe amesoma na kufaulu kidato cha nne na kujiendeleza katika vyuo vya ufundi VETA na kupata VTA Level 3 au Trade Test I.

7. Utaratibu wa kujaza fomu ya maombi
Mwombaji anaweza kuchukua fomu kutoka kwenye Kampasi (Chuo) au kwa kufungua Tovuti ya Wakala – Website: http//www.lita.go.tz na kujaza fomu na hatimaye kuzirudisha kwenye Kampasi (chuo) au kwa njia ya barua pepe zifuatazo: litahq@yahoo.com
Pamoja na fomu ya maombi ambatanisha payslip ya ada ya maombi uliyolipia kwenye akaunti ya Wakala kama ilivyoelekezwa kwenye fomuya maombi.

Zingatia: Maombi yoyote yasiyozingatia maelekezo tajwa katika tangazo hili hayatashughulikiwa
Fomu ya maombi (Application form) HAIUZWI!

8. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/08/2107.

9.Taarifa kwa watakaochaguliwa.
Majina ya watakaochaguliwa yatatolewa kwenye:
Website: http://www.lita.go.tz na magazeti ya Habari leo na Mwananchi.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
Mtendaji Mkuu,
Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo – LITA,
Veterinari Complex,
131 Barabara ya Nelson Mandela,
S. L. P 9152,
15487 Dar es Salaam
Simu Na. +255 22 28633479

Pakua fomu hapa>>>>Application-forms-LITA-2017-2018


52 Comments

  1. rashid says:

    vpi kuusu matokeo ya walio apply mwaka uu 2018/19 bdo atuja yapat

    Like

  2. johanes9 says:

    Ni Mimi mwanachuo wa tengeru Arusha mifugo nilikua naulizia kivipi kuhusu mkopo tuna ruhusiwa kuomba sisi mwaka wa pili cheti CAHP 2016 coz muda unaenda na atuna taarifa tusaidie BC
    I’m johanes

    Like

  3. jose depela says:

    naomba kuuliza kwa yule aliye pitia mafunzo ya VETA in ANIMAL HUSBANDRY na kumaliza fom four anaweza kujiunga diploma?

    Like

  4. emmanuel elias says:

    mimi nimemaliza kidato cha nne nimepata three ya 25 nimefaulu bios C na chemia D na geography nina C

    Like

  5. Magesa John says:

    kuna majina nasikia yako chuoni kwa waliochaguliwa kujiunga na chuo campuss ya mpwapwa kila kwenye mtandao hayapo. Please naomba msaada kama naweza kuyapata.

    Like

  6. hamic says:

    mim nmehitimu kidato cha nne mwaka 2015 nmepata four 32 je naweza kujiunga na chuo ngaz ya astashahada.

    Like

  7. emanuel juma says:

    Anaye jua chochote kuhusiana na ngazi ya diploma ya animal health naomba unisaidia kunitumia kwa kutumia hii email chrisantbuware@gmail.com

    Like

  8. emanuel juma says:

    Mbona page ikifunguliwa haifiki mwisho afu ngazi ya diploma majina hayaonekani naomba usaidizi

    Like

  9. evarist says:

    Mim hapa nimechaguliwa kujiunga na lita campas ya madaba na ningependa kuomba uhamisho maana kule kutakuwa mbali sana na nyumbani.naomba mwenye kuelewa zaidi kuhusu uhamisho anisaidie tafadhali.

    Like

  10. Ngwaya says:

    LIST ya majina imetoka ila haieleweki sijui haijakamilika kwa anaetaka kuiyona achek web ya lita http://www.lita.go.tz ataiyona ila sijui haijakamilika… kwa mwenye taarifa sahihi kuhusu hili atujibu tafadhali.

    Like

  11. Jaman mwenye hyo lista naomb anitumie kwenye emaili hi tafadhal). Floriankilyenyi145@gmai.com

    Like

  12. Denis Gingo says:

    jaman kwa anayejua zaid kuhusu hii list anifahamishe maana naona haijakamilika

    Like

  13. Jaman tusaidieni hiyo list wezet mumeonaj mbona hatuon

    Like

  14. Ngwaya says:

    Jamani mwenye LIST ya majina ya waliochaguliwa na LITA anitumie tafadhali kupitia email hii ngwayashalon@gmail.com

    Like

  15. Mana nimesech kweny website ya lita.go.tz cjayaona na tuliambw yatapostiw kweny hyo website

    Like

  16. Jaman mbona mi sijaona hiyo list msaada wenu tafadhali nipate kuona

    Like

  17. Ngwaya says:

    yani hawa LITA kiukweli wanaboa kupita maelezo.. dah majina yametoka List haijakamilika. mmetoa ya nn sasa. kiukweli mnakwaza sana.

    Like

  18. evarist says:

    Mbona list ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na lita haijakamilika?

    Like

  19. LITA tutarifuni bas kama kuna tatizo

    Like

  20. evarist says:

    Dah!!kwely majbu yamechelewa tatizo ni nn? tupeni taarifa jaman

    Like

  21. evarist says:

    Mbna majbu hayatoki kwa walioapply

    Like

  22. Ngwaya says:

    kwa kweli majibu ya waliochaguliwa mwaka huu yamechelewa sana kutoka. au udahili umesitishwa maana hatuelewi then na information hamtupi LITA tatizo nn lakini daah.

    Like

  23. Tuendelee kusubiri zkiwa tayari tutarifiane

    Like

  24. Kelvin epiphan says:

    Dah! Kila day nipo na google lakini wapiiii…. Inakatasha tamaaaaa

    Like

  25. Richard shaibu says:

    Jamani mi nilichelewa kufanya application sa kwa Muda huu naweza kufanya application

    Like

  26. Jaman lita majibu yatatoka lin tuliyomba mifugo

    Like

  27. Robert paul says:

    Yan ad mtu unakata tamaaa asa mnasubir nin toen kila mtu ajue msichewesheivi hii majina mnatoa lin ya walio chaguliwa

    Like

  28. Evance says:

    jaman mbna mnachelewa kulikon hayo majibu,had Leo yani hatujui tusipo chaguliwa itakuaje yani!!

    Like

  29. Ngwaya says:

    Matokeo ya waliochaguliwa yamechelewa sana mwaka huu. Tatizo nn?

    Like

  30. rahma seif says:

    matokeo ya waliochaguliwa yanatoka linii

    Like

  31. Charliè Minja says:

    Ucjal yatatoka tu nazan haitavuka tareh kumi na nne mwezi huu

    Like

  32. Ngwaya says:

    Mbona majina mwaka huu yamechelewa sana kutoka. Na yatatoka lini?

    Like

  33. Vaileth Valentine says:

    Mbona majina ya waliochaguliwa yamechelewa kutoka

    Like

  34. petro zacharia says:

    kama nisipo chaguliwa na weza kwenda kwenye chuo husika nikapokelewa na kusoma

    Like

  35. Zuhura Kilima says:

    Samahan naomba kuuliza majina ya watakaochaguliwa yanatoka lini

    Like

  36. majina ya watakaochaguliwa yanatoka tarehe gani

    Like

  37. bahati magesa says:

    nlkua nauliza majibu ya walio Fanya application yanatoka lini

    Like

  38. Kelvin Joseph mrema says:

    Mimi nilijaza fomu nikaituma kwa njia ya posta kupitia anuani niliyopata kwenye ile fomu s.l.p 9152,15487 dar es Salaam nilikua naomba kuulizaa kama nilivyo tuma nisahihi

    Like

  39. JUMA MILLANZI says:

    I need to know if there is second extension deadln on application for CAHP & DAHP n.k.

    Like

  40. emanuel juma says:

    Kutuma mumetuma taree ya mwisho ya kupost application je majibu ya kuchaguliwa ni lini yanatoka

    Like

  41. Elick Simon says:

    M nina chemistry D,biology c,geog D,kisw d,engl d,civics d,history d,je nikiaply animal health and production unapata nafas au

    Like

  42. chrisant wilbert says:

    Njia gan inatumika kupangwa chuo husika mfano tengeru na E mbili katika somo la bio na geo katika A leval mwaka 2017

    Like

  43. getruder radier says:

    good

    Liked by 1 person

Weka mawazo yako hapa