Home » Habari » MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2O17/18

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI 2O17/18

Advertisements

TAKWIMU MUHIMU:
Jumla ya watahiniwa wa shule – 349,524
wasichana – 178,775 (51.1%)
wavulana – 170,749 (48.9%)
Jumla ya watahiniwa wa kujitegemea – 47,751
wasichana – 24,587 (51.5%)
wavulana – 23,164 (48.5%)
Watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu – 96,018 (27.60%)
VIGEZO VILIVYOTUMIKA KWA MWAKA HUU:
i) AAA hadi CCD kama cut off point kwenye masomo ya tahasusi (Combination)
ii) Credit 3 na pointi zisizopungua 25 kwenye Daraja
iii) Machaguo yaliyojazwa na mwanafunzi kwenye selform.
iv) Nafasi zilizopo katika Shule husika
WANAFUNZI WENYE SIFA
Kati ya wanafunzi 96,018 ni wanafunzi 93,019 ndio wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama nilivyoainisha hapo juu.
Kati ya hao, Wanafunzi 92,998 ni wa Shule (School Candidates) na Wanafunzi 21 walisoma chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
TAREHE YA KURIPOTI
Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2017, utaanza tarehe 17 Julai 2017

lakini kwa wanafunzi wanaongia Kidato cha Sita watafungua Shule tarehe 3/7/2017 kama ilivyokuwa

imepangwa. Kwa kuwa upangaji wa wanafunzi wanaoingia Kidato cha Tano kwa mwaka 2017 umezingatia
machaguo ya wanafunzi wenyewe na nafasi zilizopo katika Shule husika, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule. Nitumie nafasi hii, kuwaagiza wanafunzi wote kuripoti katika Shule walizopangwa kwa wakati.
Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi yasiku 14 kuanzia tarehe ya kufungua Shule, nafasi yake itachukuliwa na wanafunzi wengine
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2017
inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya: http://www.tamisemi.go.tz & http://www.moe.go.tz
Aidha, fomu za kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi (joining instructions) zinapatikana kwenye shule alikopangiwa mwanafunzi na kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ya: http://www.tamisemi.go.tz
IMETOLEWA NA:
George B. Simbachawene (Mb)
WAZIRI WA NCHI, OR-TAMISEMI
Fungua link hizi hapa chini kuona majina:
Advertisements

12 Comments

 1. fellow iddy says:

  kama tutaachwa kiukweli itaniuma saana… Ukiangalia nimefaulu vzuri combi zangu zimebalance afu mwisho wacku waje kuniacha… Takua cnatofauti tena na aliyepata division 0… Wengine tulijidhulumu mpka usingiz wetu ili tusome kwa bidii tumefaulu mwisho wasiku waje watuache nyumbani kiukweli itatuumiza sana moyoni…..

  Tafadhali “Elimu Leo Blog” tunaomba mtuulizie kama orodha ya majina walio panga kama watayachagua yote au wengine wataachwa ili tuangalie plan nyingne jamani tumechoka kukaa nyumbaninyumbani we need to study bt we need to go back to school Jamani

  Like

 2. fellow iddy says:

  Hofu na mashaka yaliojuu yetu kwasisi wanafunzi tunaosubiri second selection siyo Post kutoka Bali ni je, wanafunzi wote tulio orodheshwa majina yetu second selection tutapangiwa shule woote au kunawengine wataachwa ??? Manaake kauli ya waziri Wa TAMISEMI alisema wanafunzi walio achwa ni wanafunzi 2,999.. Lakin ukija ukiangakia wanafunzi tulip pangwa majina yetu second selection tunaosubiri kupangiwa shule tupo zaidi ya wanafunzi 34,727… Sasa tunajiulza huku tukiwa nahofu kubwa kua tutachaguliwa wote au watachagua baadhi ????

  Like

 3. Goodluck says:

  Post za second selection zitatolewa lini???

  Like

 4. fellow iddy says:

  Samahani nilikua naomba kujuzwa kuwa toleo la pili litakua lini(second selection) ??? Na nivigezo vp vinavyohitajika katika second selection ??? Manaake mi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka jana na nilipata III-25 Na vigezo vyote nilikua navyo ila sikuwepo first selection… sasa ningeomb kujuzwa ili nijue kama hawata chagua tena au laaa… Kwamaana jina langu nimeliona kwenye orodha ya second selection….. Tafadhal nsombeni msaada wenu wa majibu

  Like

 5. daniel joshua says:

  wachache yn da!

  Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: