Home » 2017 » June

Monthly Archives: June 2017

Advertisements

SERIKALI YAAGIZA POSHO ZA WALIMU ZILIPWE NDANI YA SIKU SABA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki.

SERIKALI imetoa siku saba kwa ajili ya halmashauri zote kuhakikisha walimu wa hesabu, sayansi na wataalamu wa maabara waliopangwa hivi karibuni wanapewa posho za kujikimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema). Mkundi alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao walimu wa Hesabu, Sayansi na watalaamu wa maabara waliopangiwa vituo hivi karibuni. Alisema halmashauri zote zilizopokea walimu hao zinapaswa kuwapa posho za kujikimu ndani ya siku saba.

Akijibu swali la msingi la Mkundi aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa posho za mazingira magumu kwa watumishi wa maeneo ya pembezoni, alisema, “Katika kutekeleza Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha iliyopitishwa mwaka 2010, mwaka 2012/13 halmashauri 33 za wilaya ikiwemo halmashauri ya Ukerewe ziliwezeshwa kuandaa miongozo ya kutoa motosha kwa watumishi.”

Alisema kutokana na mpango huo, halmashauri 29 ziliandaa na kuwasilisha katika ofisi ya wizara hiyo miongozo iliyobainisha aina ya motisha inayohitajika. “Utekelezaji wa miongozo hiyo kwa halmashauri zote 29 ulikadiriwa kugharimu Sh bilioni 331.087 kwa mwaka na utekelezaji wa miongozo hiyo, ulitarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2013/14 na haukuanza kutokana na ufinyu wa bajeti.

Chanzo: HabariLeo

Advertisements

UTARATIBU MPYA WA WAHITIMU WA DIPLOMA WANAOTAKA KUJIUNGA NA DEGREE 2017/18

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za usajili na ithibati, mitaala na upimaji ili tuzo zitolewazo na vyuo/taasisi ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa. Kifungu cha 5 (1) (e) na (f) cha Sheria hii kinaipa mamlaka NACTE, kuanzisha tuzo mbalimbali zinazotolewa na kuhakikisha kuwa ubora wa elimu na mafunzo ya kada ya kati yatolewayo na taasisi mbalimbali yanazingatia ubora unaokusudiwa. Aidha, Kifungu cha 11, kinalitaka Baraza kuhakikisha kuwa Tuzo zitolewazo na vyuo na taasisi zote zinazoendesha mafunzo ya kada ya kati zinatambuliwa na mamlaka husika. Katika muktadha huu, kila chuo/taasisi inayotoa elimu ya ufundi inatakiwa kuwasilisha Baraza matokeo ya mitihani kila mwisho wa semista.


Hivyo, kwa kuwa Udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Shahada mbalimbali yanayotolewa na taasisi/vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, Baraza linao wajibu wa kuziwezesha taasisi/vyuo hivyo kudahili wanafunzi wenye sifa stahiki.


Ili kulifanikisha hili, Baraza limeandaa mfumo ambao taasisi/chuo kitapata taarifa za muombaji mwenye sifa linganifu (muhitimu wa Stashahada) moja kwa moja.


Hivyo, wahitimu wote wa Stashahada yoyote wanaokusudia kuomba kujiendeleza katika ngazi ya Shahada wanatakiwa kuhakiki taarifa zao Baraza (NACTE) kabla ya kufanya maombi yao kwenye taasisi/vyuo wanavyotaka kwenda kusoma. Uhakiki huo utafanywa kwa njia ya mtandao (online) kupitia Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo (NACTE Award Verification System – NAVS) kwa kubofya hapa au kupiti tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) kwa kubofya kitufe kilicho andikwa Award Verification. Baada ya kuhakiki taarifa zake kuwa kamilifu na sahihi, mhakiki atapatiwa Namba ya Utambulisho(Award Verification Number – AVN) ambayo itaambatanishwa na maombi ya Udahili kwenye taasisi/chuo husika. Utambulisho huo utatumiwa na taasisi/chuo kujiridhisha kwamba taarifa alizowasilisha muombaji wa Udahili ni sahihi na hivyo kuweza kudahiliwa na kisha kuchaguliwa kwa ajili ya masomo kulingana na mahitaji ya taasisi/chuo husika.


Aidha, Baraza linapenda pia kuwafahamisha wale wote walio na Stashahada walizopata nje ya nchi (Foreign Diploma Awards), nao waziwasilishe kupitia mfumo huu (NAVS) kwa ajili ya kuzifanyia ulinganifu na kuweka taarifa zao kwenye Kanzidata ya Baraza ili nao waweze kupata Namba ya Utambulisho. Maelezo ya namna ya kuziwasilisha tuzo za kufanyiwa ulinganifu yanapatika kwenye tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).


Ili mwombaji Udahili apate Namba ya Utambulisho atalipa Shilingi Elfu Kumi (10,000/=) kwa njia ya mtandao (Online) kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye Mfumo wa Uhakiki wa Tuzo – NAVS.  Kwa wale wanaotaka kufanya ulinganifu wa vyeti vyao, watatakiwa kulipa Shilingi Elfu Ishirini (20,000/=) kwa tuzo za ndani ambazo hazisimamiwi na baraza, na Shilingi Elfu Hamsini (50,000/=) kwa tuzo za nje ya nchi (foreign awards).


Baraza linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa wanaweza kufanya uhakiki huo kuanzia leo tarehe 28 Juni, 2017 hadi tarehe 20 Julai, 2017.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 28/06/2017

MWALIMU AJIUA KWA KUNYWA SUMU KATAVI

Habari kwa Hisani ya MPEKUZI
Mwalimu  Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa  wilayani Nkasi   amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema   mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga  karibu na kituo kikuu cha    mabasi yanayokwenda  mikoani.
Alisema hadi sasa   hakijafahamika chanzo cha mwalimu huyo kujiua kwa   sumu ingawa aliacha ujumbe uliosomeka, “Kama nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu lakini nisilaumiwe chochote juu ya kifo changu”.
Inadaiwa kwamba siku ya tukio mwalimu huyo  alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na baadaye  alikabidhi funguo na kuondoka kwenda kusikojulikana.
Taarifa zinadai   ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa akachukua ufunguo kwa mhudumu  na kuingia ndani ya chumba chake   kulala.
Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya mtu akikoroma kwa sauti ya juu hali iliyozua hofu.
Mhudumu   alilazimika kuomba msaada kwa wapangaji wengine waliokuwamo ndani ya nyumba  hiyo na  kuvunja mlango.
Baada ya kuvunjwa kwa mlango mhudumu huyo akiwa na wapangaji hao, walimkuta mwalimu huyo akiwa anatokwa mapovu hali iliyowalazimu kumkimbiza  hospitalini lakini wakiwa njiani alifariki dunia.
RPC Kyando  alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa utabibu,   Mwalimu  Sanga alikunywa sumu.

MATOKEO YA MITIHANI YA BODI YA UHASIBU (NBAA) KWA MWEZI MEI 2017

ANALYSIS OF CANDIDATES’ PERFORMANCE IN THE
85TH EXAMINATION SESSION – MAY 2017
OVERALL CANDIDATES’ PERFORMANCE
During the 85th examination session, 7,135 candidates were registered for the Board’s examinations
held in May, 2017, out of whom 521 (7.2%) candidates were absent from the examinations, 6,614
candidates sat for the examinations. Of the 6,614 candidates who sat for the examinations, 1,230
(18.6%) candidates passed while 2,599 (39.3%) candidates part passed and a total of 2,785 (42.1%)
candidates failed the examinations.

ACCOUNTING TECHNICIAN CERTIFICATE (ATEC) – LEVEL I
The May 2017 examination session was the 6th session since the review of the examinations
structure and syllabi of ATEC. 108 candidates registered themselves for the examination. 5 (4.6%)
candidates were absent. 103 candidates sat for the examination, out of whom 32 (31.1%) passed
hence becoming eligible for a STATEMENT OF SUCCESS at this level. 47 (45.6%) candidates
are part passed while a total of 24 (23.3%) candidates failed the examination.

ACCOUNTING TECHNICIAN CERTIFICATE (ATEC) – LEVEL II
This examination was conducted for the 6th time since the review of the examination structure and
syllabi of ATEC II. Out of 194 candidates who registered for the examination, 09 (4.6%) candidates
were absent leaving a total of 185 candidates who wrote the examination. 67 (36.2%) candidates
passed and hence are recommended to be issued with CERTIFICATES OF COMPLETION of
the Accounting Technician Certificate Examination. 73 (39.5%) candidates have part passed while
a total of 45 (24.3%) candidates failed the examination.

FOUNDATION LEVEL
The Foundation Level examinations consist of five subjects. These subjects were tested for the
sixth time this session following the review of the examination structure and syllabi.
In this examination, 607 candidates registered themselves for the examination out of whom 50
(8.2%) candidates were absent. Of the 557 candidates who wrote the examination, 206 (37%)
candidates passed hence becoming eligible for a STATEMENT OF SUCCESS at this level. 251
(45.1%) candidates have part passed while a total of 100 (18.0%) candidates failed the examination.

INTERMEDIATE LEVEL
The Intermediate Level examinations consist of six subjects. As with the Foundation Level
examinations, these subjects were tested for the sixth time this session following the review of the
examination structure.
In this examination, 3,813 candidates registered themselves out of whom 336 (8.8%) candidates
were absent. Of the 3,477 candidates who wrote the examination, 536 (15.4%) candidates passed
hence becoming eligible for a STATEMENT OF SUCCESS at this level. 1,437 (41.3%)
candidates have part passed while a total of 1,504 (43.3%) candidates failed the examination.

FINAL LEVEL
The Final Level examinations consist of four subjects. These examinations were tested for the
sixth time following review of the examination structure.
In this examination, 2,413 candidates registered themselves for Final Level examinations, out of
whom 121 (5.0%) candidates were absent. Of the 2,292 candidates who wrote the examination,
389 (17.0%) candidates passed, hence becoming eligible for a STATEMENT OF SUCCESS at
this Level. 791 (34.5%) candidates have part passed while a total of 1,112 (48.5%) candidates failed
the examination.

CANDIDATES QUALIFYING FOR THE PROFESSIONAL CERTIFICATE OF
COMPLETION
In this examination session, 65 candidates qualify for the certificate of completion of the ATEC
programme, comprising 21 (32.3%) female candidates and 44 (67.7%) male candidates.

The breakdown of the 65 candidates qualifying for the Accounting Technician Certificate:
· 01 (1.5%) have passed subjects that were remained in ATEC I
· 58 (89.2%) have passed ATEC II
· 06 (9.2%) have passed both ATEC II and remained subjects in ATEC I
On the other hand, 410 candidates qualify for the certificate of completion of the CPA programme,
comprising 147 (35.9%) female candidates and 263 (64.1%) male candidates.

The breakdown of the 410 candidates qualifying for the CPA (T):
· 59 (14.4%) passed both Intermediate and Final Level examinations
· 78 (19.0%) have passed Intermediate Level who had already passed Final Level
· 273 (66.6%) passed Final Level examinations this session

Kuona matokeo bofya viunganishi vifuatavyo:

atec 1

atec 2

atec list

foundation

intermediate

final

cpa list

cpa equivalent list

 

TANGAZO MUHIMU KUTOKA BODI YA MIKOPO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mara nyingine inawakaribisha wadau wake wote kuja kupata huduma mbalimbali katika maeneo ya Utoaji mikopo na Urejeshaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia leo tarehe 28 Juni hadi tarehe 08 Julai, 2017 katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Kimataifa wa J.K. Nyerere (Sabasaba), uliopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi hiki chote; Bodi ya Mikopo itatoa huduma kwa wateja katika banda lake lililomo katika banda kuu la Benjamín William Mkapa kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni. Wadau watajibiwa maswali na kupewa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Utoaji Mikopo hususan kwa Mwaka wa masomo 2016/2017 na maandalizi ya mwaka mpya wa masomo 2017/2018.

SABASABA

Kuhusu Urejeshaji wa Mikopo; Taarifa za kiasi cha mkopo anaodaiwa mnufaika zitatolewa ambapo Wanufaika ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao wataweza kujaza fomu za maulizo (inquiry forms) kwa kutoa taarifa zao za sasa ili Bodi iweze kuanza kukusanya mikopo kutoka kwao.

Kwa upande wa Utoaji mikopo; wadau watapata fursa ya kujua vigezo vinavyotumiwa, utaratibu wa kuomba hadi kupangiwa mikopo, viwango vya mikopo vinavyopangwa; utaratibu wa kukata rufaa na iwapo kuna tatizo la utoaji mikopo kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taarifa za mwombaji mkopo.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu pia imeandaa machapisho yenye taarifa za utoaji na urejeshwaji mikopo ili kuwagawia wadau watakaotembelea banda lake.

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Tarehe 28 Juni, 2017

%d bloggers like this: