Home » Habari » TANGAZO LA UDAHILI WA CERTIFICATE NA DIPLOMA KWA MWAKA 2017/2018

TANGAZO LA UDAHILI WA CERTIFICATE NA DIPLOMA KWA MWAKA 2017/2018

Advertisements

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini, utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na  vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.

Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali  utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tuyatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.

Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 10/05/2017

Advertisements

155 Comments

 1. rabi fales says:

  Hivi coz

  Like

 2. vedasto says:

  Udahilli wa wanafunzi kwenda vyuoni mwaka wa masomo 2018/19 Lini

  Like

 3. magdalena Andrew says:

  wadau naomba kufahamishwa matangazo ya kujiunga na vyuo vya kilimo ngazi ya diploma 2018/2019 yameshatoka na ni vyuo vipi?

  Like

 4. An intriguіng discᥙssion is worthh commеnt. I think that yyou should publish
  more on this іssᥙe, it mіgght not be a taboo matter Ƅut usually folҝs don’t talk about such
  issues. To the next! Best wishes!! http://www.barcodekitties.com/

  Like

 5. JOSEPH PETER says:

  nina B ya bio, D ya chem, F ya phys,na D ya math naweza jiunga na clinical officer ngaz ya diploma.

  Like

 6. Madua Hussein says:

  Nina c 3 ambazo ni history, GEOGRAPHY, ENGLISH LANGUAGE naweza nikasoma kozi gani kwa masomo hayo

  Like

 7. Raleigh says:

  I am truly thankful to the holder of this site who has shared this wonderful post
  at here.

  Like

 8. Mussa peter says:

  Ivi maombi ya kusoma diploma ya nursing kwa Sie ambao Tayar tumemaliza certificate ya nursing mwaka 2017 na matokeo tayari yametoka, ni Lin tunatuma maombi afu ninatakiwa kuwa na vigezo vip au GPA ipi ili nisome hiyo diploma

  Like

 9. 0768000475 says:

  mimi nina history d geog c na language d masomo yote ya arts d kasoro maths nina f.je naweza kuapply course itanifaa

  Like

 10. Viviane King says:

  Samahani Naomba Kuuliza Nina Chem C,bios C Phys E Je Naweza Kupata Course Ya Medical Laboratory In Diploma, Kwa Chet Cha Olevel

  Like

  • Amina says:

   Nmesoma kidato cha nne na nmepata div2 nikaendelea na frm six nikapata div 4 ya e moja naruhusiwa kuanza certfcat au diploma kw kozi ya ualimu science

   Like

 11. Lwitiko Gladson says:

  habari ninaomba kusaidiwa, inawezekana mtu kunbadiri course toka BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE IN COMMUNITY HEALTH kwenda BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE IN NURSING? naomba msaada.

  Like

 12. naomba kuuliza Mimi Nina chem D bios C na phy F naweza kupata kozi katika vyuo vya afya

  Like

 13. Liberatus Michael says:

  hv haya majina ya wanafunzi wa certificate in nursing Co na medical lab yashatangazwa?

  Like

 14. Benson says:

  Naomba kuuliza mm nmemaliza kidato cha sita na nmepata dvsion 3-13 nna DDE… Na nmeomba bachelor of laboratories technician… Na nyngne nyng… Je ntapata chuo???

  Like

 15. said says:

  Hi guys hiv kujiunga na ngazi ya diploma kutoka certificate ni vigezo gani wanataka

  Like

 16. miss anthony says:

  Naomba msaada nina dv 4 point 28 ya art je naweza kujiunga na chuo cha kilimo

  Like

 17. Moses peter says:

  Jaman mm Nina ,biology C, chemistry D,physics C, mathematics,D, ninaruhusiwa kuchukua diploma ya nursing

  Like

 18. Martin Kisuba says:

  Nina C chemistry, B bios ,But Physics Nina E vip naruhusiwa omba teaching au Clinical Medicine courses..?

  Like

 19. Abel M Hamis says:

  min nina C,,ya bio na chemistry na B ya English na F hesbu,,,,nlikua nataka kusomea clinical officer,,,je naruhusiwa?

  Like

 20. Liberatus Robert says:

  Samahan nilikuwa naomba kuuliza mim nina C ya Bio,D ya Geo F ya Chem nlkua nmechukua Comb CBG dv iii ya 24 eti naruhusiwa kusomea sayansi ntakapochaguliwa kujiunga na chuo cha ualimu ngaz ya diploma nmemalza shule 2015 halafu udahili unafanyika kupitia nacte au moja kwa moja chuoni?

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Hilo la kuruhusiwa kusoma Sayansi linaweza kujibiwa vyema chuoni unakotaka kusoma. Kuhusu maombi, kwa vyuo binafsi unaomba moja kwa moja chuoni ila kwa vyuo vya serikali unaomba kupitia NACTE

   Like

  • Maiko Edmund Fedelis says:

   I completed form 4 last year, after declaration of results like scored division 2. But I would like to join with primary teaching course, I have a lot of reasons to so. Honestly I really like to teach primary school especially bush schools, Am I allowed to apply for this field regardless my points?

   Like

  • Maiko Edmund Fedelis says:

   I completed form 4 last year, after declaration of our results I scored division 2. But I would like to join with primary teaching course, I have a lot of reasons to so. Honestly I really like to teach primary school especially bush schools, Am I allowed to apply for this field, regardless my points?

   Like

 21. Mimi wakuu napenda kuuliza hivi kozi ya kuhifadhi kumbu kumbu za afya ngazi ya stashahada inafundishwe kwenye chuo cha bukumbi?

  Like

 22. mulhat says:

  Tafadhali naomba ufafanuzi kwa wale walimu wenye certificate watumie njia gani kujiendeleza?? Kwa kuwa dipaloma in primary education haipo?,

  Like

 23. Eston says:

  Ninauliza hivi diploma yoyote ila ni lini wataanza pewa mikopo ya elimu ka ilivyoahidiwa na mweshimiwawezi wa kwanza mwaka huu

  Like

 24. msaada. kuna chuo nmekichagua nahtaji kubadilisha niweke kingine, je inawezekana au kutatokea shida.

  Like

 25. Ikiwa Mfumo Umesha Funguliwa Lakin Kada Unayo Ombea Kupitia Mtandao Inagoma Kuja Wanaleta Kada Moja Ty, Nin Tatzo? Na Taratibu Zote Tayali Had Kulipia Nacte? Nimeombea Ualim Inagoma Kada Iyo Kuja Naomba Msaada Wakuu Kuusu Ili,,,

  Like

 26. Frank says:

  Lini vyuo vitafunguliwa vya ualimu ?

  Like

  • naombamsaada wakuu niemeendaku apply kwa internet cafe kupitia mtandao leo tar28 process zote zimefanyika hadikulipia hela nlikua naombeakada yaualimu lakin imekuja kugomamwishokwenyeuchaguz wa kadawana leta kada ya health bas ualimu nayoombea hawa lete nin tatizo ,? msaaadaa jamaan!!!

   Like

 27. Frank says:

  Lini vyuo vitafunguliwa vya ualimu ?

  Like

 28. Renatus Joachim says:

  kama uliomba udahili wa mwezi wa tatu na ukachaguliwa ila ukashindwa kujiunga na hayo masomo je kwa sasa naweza kutuma tena maombi na kwa njia ipi sababu jina tayari lisha chaguliwa.

  Like

 29. saiman mollel says:

  Mimi Nina mdogo wangu ana dv ya 26 je anawezapata nafasi na kwa baati mbaya chet chake cha kuzaliwa kina jina twafwaut na na jina la shulen je nifanyeje niweze kusolvu

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Aende mahakamani aapishwe kuwa majina yote ni ya kwake au aende RITA abadilishe cheti cha kuzaliwa

   Like

 30. menas says:

  Naomba orodha ya vyuo vya diploma ya sekondar kwa masomo ya arts

  Like

 31. patrick geay says:

  Samahanini jaman hiv kwa wale 2liorisit mtihani 2naruhusiwa kujiunga na vyuo vya afya kwa ku2mia original chet na cha kurisit hata kama nina vigezo? Japo kwa kuunga vyeti

  Like

 32. Thomas keng'anya says:

  nikiapply kutmia smart phone ntafanikiwa

  Like

 33. Tiko says:

  Kwa Mtu aliepata dv two ya 18 na Ana D Physics D Chemistry na B biology na Mwenye dv two ya 20 na Ana C physics C biology Na D ya Chemistry anaweza pata diploma ya Phamaciutical au Medical laboratory?

  Like

 34. halson kanyondwi says:

  naomba anaejua sifa za kujiunga na ualimu ngazi ya chet 2017/2018 anisaidie please

  Like

 35. jamani mimi nina physics d chemistry c na biology c je naweza pata chuo cha afya

  Like

 36. rouben gideon says:

  samahni jaman naombeni msaada,hivi kwa hapa daresalaam ni vyuo gani vya serikali vinavyotoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya diploma??

  Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: