Home » Habari » MAJINA YA WALIMU WA SAYANSI WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI

MAJINA YA WALIMU WA SAYANSI WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI

Advertisements

Serikali imeajiri walimu wapya 3,081 na watatakiwa kuripoti kuanzia Aprili 18, 2017. Bado kuna nafasi za walimu 1,048 zilizotolewa kibali cha ajira.

Waziri wa TAMISEMI, George Simbachaweni amesema kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo ya sayansi na hisabati na kuna ziada ya walimu 7,463 wa masomo ya sanaa.

Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.

Wizara pia imetoa angalizo kwa walimu hao kama ifuatavyo:-

i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.
ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.
iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.
v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.

Fuata link hapo chini kuona majina ya walimu walioajiriwa na vituo vyao vya kazi walivyopangiwa

Majina ya walimu wenye shahada za sayansi waliopangiwa vituo vya kazi

Majina ya walimu wenye stashahada za sayansi waliopangiwa vituo vya kazi

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: