Home » 2017 » April

Monthly Archives: April 2017

Advertisements

MAJINA YA WALIMU WA SAYANSI WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI

Serikali imeajiri walimu wapya 3,081 na watatakiwa kuripoti kuanzia Aprili 18, 2017. Bado kuna nafasi za walimu 1,048 zilizotolewa kibali cha ajira.

Waziri wa TAMISEMI, George Simbachaweni amesema kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo ya sayansi na hisabati na kuna ziada ya walimu 7,463 wa masomo ya sanaa.

Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.

Wizara pia imetoa angalizo kwa walimu hao kama ifuatavyo:-

i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.
ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.
iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.
v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.

Fuata link hapo chini kuona majina ya walimu walioajiriwa na vituo vyao vya kazi walivyopangiwa

Majina ya walimu wenye shahada za sayansi waliopangiwa vituo vya kazi

Majina ya walimu wenye stashahada za sayansi waliopangiwa vituo vya kazi

Advertisements

WATU KUMI WENYE AKILI (IQ KUBWA) KULIKO WOTE DUNIANI

Kipimo cha IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa kawaida binadamu wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea. Leo nimekuletea hii list ya watu kumi wanaoaminikia kuwa na akili hadi kufikia mwaka 2017.

1: Terrence Tao

Ni mwanahisabati kutoka Marekani ambaye anakadiriwa kuwa na IQ level ya 230. Terence Tao aliweza kufanya hisabati akiwa na miaka 2 na alipokuwa na miaka 7 aliweza kufanya hesabu ngumu za level ya Chuo Kikuu akiwa na miaka 20 alipata PhD. Mwaka 2006 alishinda medali  ya Field na mwaka 2014 alipata tuzo ya Breakthrough prize in mathematics.

2: Christopher Hirata

Ni Mnajimu aliyebobea katika mambo ya anga ambapo kwa sasa anafanya kazi katika Shirika la Mambo ya Anga la Marekani ‘NASA’. Anatajwa kuwa na IQ level ya 225 ambapo akiwa na miaka 13 alipata tuzo ya Mwanahisabati Bora wa Dunia  na kuweza kupata PhD akiwa na umri wa miaka 22.

3: Kim-Um -Young

Anachukua namba 3 kati ya watu wenye akili duniani akiwa na IQ level 210 ambapo mwaka 1990 Kim Ung–yong alishika rekodi ya Dunia ya Guiness kwa kuwa na IQ kubwa. Alipokuwa na na miezi 6 tu Kim Ung-Yong  alikuwa anajua kuongea na alipofikisha miaka 3 aliweza kuongea Kijapan, Kikorea, Kiingereza na Kijerumani.

4: Rick Rosner

Watu wengi hawakuamini baada ya Rick Rosner kugundulika kuwa na IQ level ya 192 kwa kuwa kazi alizokuwa anazifanya hazikuendana na akili yake. Kabla ya kuwa mwandishi wa kipindi cha Jimmy Kimmel Rick Rosner alikuwa dansa wa club za usiku, model na waiter.

5: Garry Kasaporov

Garry ana IQ level ya 192 na ameweka rekodi ya Mchezaji Bora wa Chess Duniani kwa sasa anajihusisha na siasa kwa kiasi kikubwa ambapo alitaka kugombea Urais wa Urusi dhidi wa Raisi wa sasa Vladmir Putin.

6: Galileo Galilei

Licha ya kuwa mwanasayansi mkubwa aligundua mambo mbalimbali ya Anga , Hisabati na Fizikia. Galileo ameshika namba 6 kati ya watu wenye akili duniani akiwa na IQ level ya 185. Hadi kufikia mwaka 2017 Mwanasayansi huyu hajatoka kwenye top ten na anajulikana zaidi kwa ugunduzi wake wa umbo la dunia.

7: James Woods

Ni mcheza filamu kutoka Marekani ambaye ameshinda tuzo mbalimbali za Academy na anatajwa kuwa na IQ level ya 180. Akiwa na umri mdogo Jamaes alikuwa anaweza kufanya hesabu ngumu  licha ya uwezo wake wa mambo ya Sayansi Garry aliamua kuwa mcheza sinema.

8: Judit Polger

Ni mwanamke pekee kwenye list hii hadi kufikia mwaka 2017. Judith anatajwa kuwa na IQ level ya 170 akiwa na miaka 15 tu aliweza kumshinda mshindi wa dunia kwenye mchezo wa chess.

9: Sir Endrew Willes

Ni mwanahisabati na mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Marekani ambapo anatajwa kuwa na IQ level ya 170. Andrew Wiles aliweza kukokotoa hesabu ngumu zaidi duniani zinazoitwa Fermat’s Last Theorem na mwaka 2016 alishinda tuzo ya Abel Prize.

10: Albert Einstein

Ukitaja jina la Eistein untakuwa unamaansiha “Genious” ambapo mwanafizikia huyu ameweza kujijengea jina kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya Sayansi na mambo ya Anga. Einstein anatajwa kuwa na IQ level ya 160.

Habari kwa hisani ya MillardAyo.com

%d bloggers like this: