Home » Habari » UFAFANUZI WA TCU JUU YA TAARIFA ZA UHAKIKI WA WANAFUNZI

UFAFANUZI WA TCU JUU YA TAARIFA ZA UHAKIKI WA WANAFUNZI

Advertisements

tcu-june1

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefafanua kuwa si wanafunzi wote iliyowaorodhesha kwa madai ya kutokuwa na sifa katika programu walizodahiliwa, hawana sifa hizo isipokuwa kuna dosari katika taarifa zao.

Imebainisha kuwa baada ya uhakiki wa hivi karibuni katika baadhi ya vyuo vikuu, ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8 wana sifa stahiki na jumla ya wanafunzi 8,167 sawa na asilimia 6.2 walibainika kuwa na kasoro katika taarifa za sifa zao.

Kutokana na hilo, imewataka wanafunzi wote waliorodheshwa na tume hiyo kuwa hawana sifa watulie na kuendelea na masomo yao hadi pale dosari hizo zitakapofanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Eleuther Mwageni, tangu TCU itoe taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa uhakiki katika vyuo 52 na takribani wanafunzi zaidi ya 8,000 kugundulika kuwa hawana sifa, taarifa hiyo imepokelewa kwa mitazamo na hisia tofauti na kusababisha mkanganyiko vyuoni.

Alisema kwa kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali, TCU sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha uhakiki huo.

“Tume ilitoa taarifa kwa umma kuwaomba wanafunzi kurekebisha dosari hizo kwa kuthibitisha taarifa zao kupitia vyuo husika ifikapo Februari 28, mwaka huu ili kuweka kumbukumbu sahihi za mwanafunzi,” amesema Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU.

“Hivyo wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao kama kawaida. Pia ifahamike kuwa wanafunzi waliorodheshwa siyo kwamba wamethibitika kuwa hawana sifa stahiki, bali kuna dosari katika taarifa zao,” amesisitiza.

Alisema uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa Kifungu 5(1)(b)(c) cha Sheria ya Vyuo Vikuu Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.

Alisema katika kutekeleza jukumu hilo tume hiyo ilianza uhakiki kuanzia Agosti mwaka jana na hadi kufikia Februari mwaka huu, ilikamilisha uhakiki kwa vyuo 67 kati ya 84 vinavyotoa shahada ya kwanza.

“Hii ni mara ya kwanza uhakiki wa sifa za wanafunzi wa vyuo vyote nchini kufanyika kwa wakati mmoja. Lengo la uhakiki lilikuwa kujiridhisha kuwa wanafunzi waliopo vyuoni ni wale waliodahiliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu na kwamba wanakidhi vigezo stahiki,” alifafanua mtendaji huyo.

Alisema uhakiki ulifanyika kwa kulinganisha taarifa za TCU na zile zilizowasilishwa na vyuo. Uhakiki huo ulihusisha jumla ya wanafunzi 131,994 waliopo vyuoni kwa mwaka wa masomo 2016/17.

Aidha, alisema baada ya kulinganisha orodha zilizowasilishwa na vyuo na ile ya TCU, ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8 wana sifa stahiki na jumla ya wanafunzi 8,167sawa na asilimia 6.2 walibainika kuwa na kasoro katika taarifa za sifa zao.

Baada ya TCU kutoa majina ya wanafunzi wasio na sifa katika programu walizodahiliwa vyuoni, baadhi ya vyuo vilivyotajwa kuwa na wanafunzi hao kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, viliibuka na kudai havina mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa bila kuwa na sifa.

Naibu Makamu Mkuu wa Udsm, Profesa Florens Luoga alisisitiza kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaotaka mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema alisema wao walipelekewa taarifa na TCU kwamba kunatakiwa kufanyika kwa uhakiki wa wanafunzi wao na miezi miwili iliyopita wakaandaa taarifa hizo na kuziwasilisha kwao.

Alisema alishangaa kuona idadi ya wanafunzi 476 na kuambiwa kuwa hawana sifa na kusisitiza kuwa ni makosa kusema wanafunzi hao hawana sifa wakati wanakidhi vigezo.

Alisema lakini hawafanyi kazi za kurudi nyuma na kuangalia usahihi kama walikuwa wamekosa sifa na wakawachukua kinachotakiwa kwa sasa ni kuangalia hatua gani zichukuliwe. Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Dk Padri Thadeus Mukamwa ambacho TCU imebainisha kuwa na wanafunzi 1,046 wasiokuwa na sifa, alisisitiza taarifa hiyo ya TCU ni ya uonevu na imekiharibia sifa chuo hicho.

Alisema TCU ina sheria zake na kabla ya kuwatangaza wanafunzi hao, walitakiwa kuweka bayana kwamba tume hiyo ndio iliyokosea kwa kuwa udahili wote umefanywa na wao wenyewe. Alisema walikuwa na utaratibu hata kabla majina hayo hayajapitishwa na TCU wanakutana wakuu wote wa vyuo vyote nchini jijini Dar es Salaam, wanafanya mkutano wa pamoja na majadiliano kwa kuangalia historia ya vyuo vyao na kisha kudahili wanafunzi.

Chanzo: HabariLeo

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: