Home » 2017 » March

Monthly Archives: March 2017

Advertisements

VIDEO FUPI: MWANAFUNZI WA ILBORU ATENGENEZA ROBOTI

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ilboru iliyopo Jijini Arusha akionesha namna ‘Roboti’ alillolitengeneza likifanya kazi.

Kijana huyo ambaye jina lake bado halijapatikana ametengeneza ‘Roboti’ hilo kwa vifaa mbalimbali ambavyo vingi si rasmi kama inavyoonekana kwenye video hiyo.

Chanzo: Jamii Forum.

Advertisements

MATOKEO YA UDAHILI WA CERTIFICATE NA DIPLOMA KWA AWAMU YA MWEZI MACHI NA APRIL 2017

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA(CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)

KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi liliratibu zoezi la udahili kwa waombaji wa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kuanzia tarehe 23 Februari, 2017. Zoezi la maombi ya udahili lilifungwa rasmi tarehe 06 Machi 2017 ili kuruhusu uteuzi wa kwa waombaji wa kozi hizo.


Baraza linapenda kuwaarifu waombaji wa kozi za Astashahada na Stashahada; na umma kwa ujumla kuwa, matokeo kwa waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali yametangazwa tangu tarehe 25 Machi 2017kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) uliotumika kufanya maombi ya udahili. Waombaji wanashauriwa kutembelea kurasa zao (profiles) za kuombea udahili kupitia CAS ili kuona kama wamechaguliwa.


Ili kutembelea ukurasa wako, waweza pia kubofya hapa.


Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

Tarehe: 26 Machi, 2017

NAFASI ZA MASOMO KWA UDHAMINI WA SERIKALI NA TAASISI YA DONBOSCO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU TAARIFA KWA UMMA MAOMBI YA NAFASI 820 ZA MAFUNZO YA STADI ZA KAZI KATIKA SEKTA ZA TEHAMA, UJENZI, UZALISHAJI NA NGUO

 1. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Ofisi imeingia makubaliano na taasisi ya Don Bosco Net Tanzania iliyopo Osterbay, Dar es salaam ya kutoa mafunzo katika fani za Ushonaji Nguo, ufundi Bomba,Useremala, uchomeleaji, utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi wa Kompyuta (Computer maintanance and upgrading/Basic and advance microsoft office suite/web &Graphic design).

 2. Ofisi inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani tajwa hapo juu wawasilishe maombi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Don Bosco Net Tanzania.

Jumla ya Vijana 820 watafadhiliwa na Serikali kwa kulipiwa ada na nauli ya kuhudhuria mafunzo yatakayofanyika katika vyuo vya Don Bosco, Dar es salaam. Mwanafunzi atatakiwa kujigharamia malazi na mahitaji mengine ya kujikimu. Mafunzo yataanza Mwezi Aprili, 2017 na yatafanyika katika vyuo vya Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania.

Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 18/03/2017 hadi 30/03/2017 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:

(i) Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe;

(ii) Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu

(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura;

(iv) Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji; na

(v) Picha nne za paspoti.

 1. Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni Elimu ya Msingi au zaidi kwa fani za Ushonaji Nguo, ufundi Bomba,Useremala, uchomeleaji, utengenezaji wa vipuri vya mitambo; na elimu ya Sekondari kwa fani za Ufundi wa Kompyuta (Computer maintanance and upgrading/Basic and advance microsoft office suite/web &Graphic design).

 2. Maombi yawasilishwe kwa Mkurugenzi TAASISI, ya DON BOSCO NET TANZANIA, S.L.P. 32770, DAR ES SALAM au kupitia barua pepe: jpotz@dbtz.org au yawasilishwe katika vyuo vya Don Bosco Net Tanzania vilivyo katika miji ya MOSHI, DODOMA, SHINYANGA, MAFINGA NA DAR ES SALAAM.

 3. Watakaokidhi vigezo na Sifa wataitwa kuanza mafunzo kupitia magazeti na simu kuanzia tarehe 10 April, 2017.

 4. Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)

IMETOLEWA NA: KATIBU MKUU

15/03/2017

AJIRA ZA WALIMU WA HISABATI NA SAYANSI

TANGAZO KWA UMMA

NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI WALIOHITIMU MWAKA 2014/2015 KURUDI NYUMA.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia wahitimu wote wa Stashahada na Shahada ya Ualimu katika masomo ya Sayansi na Hisabati wa mwaka 2014/ 15 na miaka ya nyuma, kuwa bado kuna nafasi za ajira, hivyo, wenye sifa watume maombi yao.

Wahitimu walioomba wakati Wizara ilipotangaza nafasi za ajira mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 wasiombe tena kwa kuwa mchakato wa ajira kwa wale wenye sifa unaendelea. Wahitimu walioajiriwa Serikalini wasiombe.

Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa ni hizi zifuatazo:-

 • Elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Sita);
 • Taaluma ya Ualimu (Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu -PGDE);
 • ‘Academic Trascript’ ya Stashahada, Shahada au Stashahada ya Uzamili katika Elimu-PGDE);
 • Cheti cha Kuzaliwa;
 • Wasifu (CV) unaoonesha majina matatu. Mwombaji ambaye vyeti vyake vya Elimu na Taaluma havina jina la tatu, akamilishe taratibu za kisheria za kuongeza jina la tatu na kuwasilisha kiapo stahiki pamoja na maombi yake.

UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-

 1. Mwombaji anatakiwa ‘ku-scan’ vyeti/nyaraka halisi – (Kidato cha 4, 6, Stashahada, Stashahada ya Uzamili na Shahada) na siyo kivuli (photocopy) na kuhifadhi katika ‘File’ moja la ‘pdf’. File lipewe majina matatu ya mwombaji kuanzia la kwanza, kati na la mwisho ndipo litumwe.
 2. Mwombaji atumie anuani ya barua pepe yake mwenyewe na siyo ya mtu mwingine kutuma nyaraka zake.

TANBIHI:

 1. Tarehe ya mwisho kupokea nyaraka ni 30 Machi, 2017.
 2. Barua pepe za kuwasilisha nyaraka za waombaji zitumwe mara moja tu na si kwa kurudia rudia ili kuepuka usumbufu.
 3. Yeyote ambaye vyeti vyake havitahakikiwa hatafikiriwa katika ajira.
 4. Wahitimu ambao waliomba awali mwezi Desemba, 2016 na Januari, 2017 na nyaraka zao ziliwasilishwa kikamilifu na kupokelewa, majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya Wizara www.moe.go.tz. Hao wasiwasilishe nyaraka hizo tena.
 5. Tangazo hili haliwahusu wahitimu waliofaulu mtihani mwaka wa masomo 2015/16 baada ya kurudia masomo waliyoshindwa mwaka 2014/15.
 6. Nyaraka zote ziwasilishwe kwa barua pepe ifuatayo: apa@moe.go.tz

IMETOLEWA NA

Tarish M.K.
KATIBU MKUU
10/03/2017

UFAFANUZI WA TCU JUU YA TAARIFA ZA UHAKIKI WA WANAFUNZI

tcu-june1

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefafanua kuwa si wanafunzi wote iliyowaorodhesha kwa madai ya kutokuwa na sifa katika programu walizodahiliwa, hawana sifa hizo isipokuwa kuna dosari katika taarifa zao.

Imebainisha kuwa baada ya uhakiki wa hivi karibuni katika baadhi ya vyuo vikuu, ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8 wana sifa stahiki na jumla ya wanafunzi 8,167 sawa na asilimia 6.2 walibainika kuwa na kasoro katika taarifa za sifa zao.

Kutokana na hilo, imewataka wanafunzi wote waliorodheshwa na tume hiyo kuwa hawana sifa watulie na kuendelea na masomo yao hadi pale dosari hizo zitakapofanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Eleuther Mwageni, tangu TCU itoe taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa uhakiki katika vyuo 52 na takribani wanafunzi zaidi ya 8,000 kugundulika kuwa hawana sifa, taarifa hiyo imepokelewa kwa mitazamo na hisia tofauti na kusababisha mkanganyiko vyuoni.

Alisema kwa kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau mbalimbali, TCU sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo katika kukamilisha uhakiki huo.

“Tume ilitoa taarifa kwa umma kuwaomba wanafunzi kurekebisha dosari hizo kwa kuthibitisha taarifa zao kupitia vyuo husika ifikapo Februari 28, mwaka huu ili kuweka kumbukumbu sahihi za mwanafunzi,” amesema Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU.

“Hivyo wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo yao kama kawaida. Pia ifahamike kuwa wanafunzi waliorodheshwa siyo kwamba wamethibitika kuwa hawana sifa stahiki, bali kuna dosari katika taarifa zao,” amesisitiza.

Alisema uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa Kifungu 5(1)(b)(c) cha Sheria ya Vyuo Vikuu Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.

Alisema katika kutekeleza jukumu hilo tume hiyo ilianza uhakiki kuanzia Agosti mwaka jana na hadi kufikia Februari mwaka huu, ilikamilisha uhakiki kwa vyuo 67 kati ya 84 vinavyotoa shahada ya kwanza.

“Hii ni mara ya kwanza uhakiki wa sifa za wanafunzi wa vyuo vyote nchini kufanyika kwa wakati mmoja. Lengo la uhakiki lilikuwa kujiridhisha kuwa wanafunzi waliopo vyuoni ni wale waliodahiliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu na kwamba wanakidhi vigezo stahiki,” alifafanua mtendaji huyo.

Alisema uhakiki ulifanyika kwa kulinganisha taarifa za TCU na zile zilizowasilishwa na vyuo. Uhakiki huo ulihusisha jumla ya wanafunzi 131,994 waliopo vyuoni kwa mwaka wa masomo 2016/17.

Aidha, alisema baada ya kulinganisha orodha zilizowasilishwa na vyuo na ile ya TCU, ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8 wana sifa stahiki na jumla ya wanafunzi 8,167sawa na asilimia 6.2 walibainika kuwa na kasoro katika taarifa za sifa zao.

Baada ya TCU kutoa majina ya wanafunzi wasio na sifa katika programu walizodahiliwa vyuoni, baadhi ya vyuo vilivyotajwa kuwa na wanafunzi hao kikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, viliibuka na kudai havina mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa bila kuwa na sifa.

Naibu Makamu Mkuu wa Udsm, Profesa Florens Luoga alisisitiza kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaotaka mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema alisema wao walipelekewa taarifa na TCU kwamba kunatakiwa kufanyika kwa uhakiki wa wanafunzi wao na miezi miwili iliyopita wakaandaa taarifa hizo na kuziwasilisha kwao.

Alisema alishangaa kuona idadi ya wanafunzi 476 na kuambiwa kuwa hawana sifa na kusisitiza kuwa ni makosa kusema wanafunzi hao hawana sifa wakati wanakidhi vigezo.

Alisema lakini hawafanyi kazi za kurudi nyuma na kuangalia usahihi kama walikuwa wamekosa sifa na wakawachukua kinachotakiwa kwa sasa ni kuangalia hatua gani zichukuliwe. Kwa upande wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Dk Padri Thadeus Mukamwa ambacho TCU imebainisha kuwa na wanafunzi 1,046 wasiokuwa na sifa, alisisitiza taarifa hiyo ya TCU ni ya uonevu na imekiharibia sifa chuo hicho.

Alisema TCU ina sheria zake na kabla ya kuwatangaza wanafunzi hao, walitakiwa kuweka bayana kwamba tume hiyo ndio iliyokosea kwa kuwa udahili wote umefanywa na wao wenyewe. Alisema walikuwa na utaratibu hata kabla majina hayo hayajapitishwa na TCU wanakutana wakuu wote wa vyuo vyote nchini jijini Dar es Salaam, wanafanya mkutano wa pamoja na majadiliano kwa kuangalia historia ya vyuo vyao na kisha kudahili wanafunzi.

Chanzo: HabariLeo

%d bloggers like this: