Home » Habari » TAARIFA RASMI: NACTE WAFUNGUA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA INTAKE YA MACHI NA APRILI

TAARIFA RASMI: NACTE WAFUNGUA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA INTAKE YA MACHI NA APRILI

Advertisements
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:

 1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
 2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
 3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.

Sifa za muombaji

 1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
 2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
 3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).

Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:

 1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
 2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
 3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.

Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.


Bofya hapa kufanya maombi


BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA VYUO

Imetolewa na:

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

23 Januari, 2017

Advertisements

19 Comments

 1. Irene says:

  Je, vyuo vya maendeleo ya jamii vimesha anza udahili wa mwaka wa masomo 2018/2019?

  Like

 2. Mulhat says:

  Udahili wa kada ya elimu lini??? Mwez Wa tano ndio huu

  Like

 3. Mulhat says:

  Mie nataka taarifa za udahili kada ya elimu,,, halafu hizo taarifa zimesha expire ndio zinanifikia kma ningekuwa mlengwa mngenisaidiaje

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Habari Mulhat!
   Unaweza kurudia swali lako vizuri, una maanisha udahili wa walimu umekwisha fungwa?

   Like

 4. Mfumo Wa Udahili Utafunguliwa Lini Tena Kwa Mwaka Wamasomo 2017/2018

  Like

 5. mulhat says:

  Udahili katika kada ya elimu lini?? ?tujuzeni mapema

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Kwa kawaida huwa ni may, ila tuendelee kusubili mamlaka husika NACTE watakapofungua dirisha la udahili tutawajulisha.

   Like

 6. Emmanuel Mshashy says:

  Mimi naomba kujua kama kutakuwa na udahili mwingine katika vyuo vya kilimo kwa ngazi ya Diploma mwaka 2017/2018?

  Like

 7. lemile says:

  je kwa wale walioitim kidato cha nne 2016 udahili wao ni lini

  Like

 8. Sabinius john says:

  kwa wahitimu wa kidato cha nne 2016 wanatakiwa kuanza kufanya maombi ya kudahiliwa mda gani? .na nilini wanatakiwa kuanza kufanya maombi?

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Waliomaliza 2016 watadahiliwa mwezi wa kumi, tarehe ya kutuma maombi itatangazwa na mamlaka husika (NACTE). Endelea kututembelea utapata taarifa watakapofungua dirisha la udahili

   Like

   • Sabinius john says:

    mbona nasikia kuna baadhi ya vyuo vilivyo sajiliwa na (NACTE) pia vina Dahili wanafunzi mwezi wa saba (7)
    mfano: chuo cha JORDAN UNIVERSITY COLLEGE (morogoro)
    Au kila chuo kinataratibu zake za kudahili wanafunzi???

    Like

 9. Wiston R mtandamo says:

  napendekeza mngetoa kitabu cha muongozo waombaji wakione kabla hawaja anza kuomba pia naomba kutumiwa vigezo vya kujiunga na nursing pamoja na pharmacy kwa wanaohitaji kusoma ngaz ya cheti

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Kozi yoyote ya cheti inahitaji uwe na ufaulu usiopungua D nne za kidato cha nne, kwa msaada zaidi bofya “Kutafuta chuo/shule” kwenye menyu yetu hapo juu

   Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: