Home » Matangazo » TANGAZO KWA WAHITIMU WA SHAHADA NA STASHAHADA ZA UALIMU (SAYANSI) WALIOTAKIWA KUWASILISHA VYETI

TANGAZO KWA WAHITIMU WA SHAHADA NA STASHAHADA ZA UALIMU (SAYANSI) WALIOTAKIWA KUWASILISHA VYETI

Advertisements

TAREHE 12/12/2016 WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO KWA AJILI YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.

WAHITIMU WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-

(1) WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA AU SHAHADA

(2) WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION – PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;

WAHITIMU AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.

WAHITIMU AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI .

orodha ya wahitimu wa shahada waliokamilisha vyeti

orodha ya wahitimu wa stashahada waliokamilisha vyeti

WAHITIMU WALIOPO KWENYE ORODHA HAPO JUU WASIWASILISHE NYARAKA HIZO TENA.

UTARATIBU WA KUTUMA VYETI NI KAMA IFUATAVYO:-

  1. WAOMBAJI LAZIMA ‘WA-SCAN’ VYETI HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES – KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA, STASHAHADA YA UZAMILI AU SHAHADA) NA SIYO KIVULI CHA CHETI (PHOTOCOPY) ;
  2. WAOMBAJI WA STASHAHADA YA UZAMILI (PGDE) NA SHAHADA LAZIMA ‘WA-SCAN’ NA KUTUMA NAKALA ZA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZA SHAHADA YA KWANZA.
  3. WAOMBAJI LAZIMA WAWEKE NAKALA ZA VYETI VYAO VYOTE KWENYE ‘FILE’ MOJA LIKIWA KATIKA ‘PDF’ NA LIPEWE JINA LA MWOMBAJI HUSIKA KABLA YA KUTUMA. NYARAKA ZITUMWE KUPITIA ‘BARUA PEPE’ ZAO WENYEWE NA SIYO ZA WATU WENGINE.

TANBIHI:

  1. WAOMBAJI WATUME TAARIFA ZAO KUPITIA BARUA PEPE YA WIZARA info@moe.go.tz
  2. TAREHE YA MWISHO KUPOKEA NYARAKA NI 17 JANUARI,2017.
  3. BARUA PEPE ZA KUWASILISHA NYARAKA ZA WAOMBAJI ZITUMWE MARA MOJA TU NA SI KWA KURUDIA RUDIA ILI KUEPUKA USUMBUFU WA KUTAFUTA ZILIZO SAHIHI.

IMETOLEWA NA

PROF. SIMON S. MSANJILA

KAIMU KATIBU MKUU

12/01/2017

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: