Home » 2017 » January

Monthly Archives: January 2017

Advertisements

ANGALIA HAPA ORODHA YA VYUO VILIVYORUHUSIWA KUDAHILI DIPLOMA NA CERTIFICATE KWA MWEZI MACHI NA APRILI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

ORODHA YA VYUO VILIVYO RUHUSIWA KUDAHIRI WANAFUNZI KWA

KIPINDI CHA MARCH / APRIL, 2017 KWA MWAKA WA

MASOMO 2016 / 2017


BOFYA HAPA KUPATA ORODHA HIYO

Advertisements

TAARIFA RASMI: NACTE WAFUNGUA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA INTAKE YA MACHI NA APRILI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi

Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:

  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.

Sifa za muombaji

  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).

Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:

  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.

Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.

Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.


Bofya hapa kufanya maombi


BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA VYUO

Imetolewa na:

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

23 Januari, 2017

WANAOSOMA STASHAHADA (DIPLOMA) KUANZA KUPEWA MIKOPO

ndalichako

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako

SERIKALI imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa nafasi ya kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati mikopo.

“Kwa lengo la kupata balance (mizania) na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye elimu ya juu, watoto ni wale wale. Kuna wengine nao wanashindwa kumudu gharama na ili serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na marekebisho ya sheria,” alieleza Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako alisema kuna umuhimu mkubwa wa kada ya Stashahada, hasa wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa ujenzi wa taifa la vijana, kama ilivyo kwa wenye Shahada.

“Kama taifa tunazungumzia uchumi wa viwanda,wadau wote hata wale wa ngazi ya kati ni muhimu katika kuhakikisha kwamba ajenda hii inafanikiwa kama vile ambavyo wale wa digrii wangelifanya,” aliongeza waziri huyo.

Mwaka 2004, kulikuwepo na mabadiliko katika sheria hiyo iliyowezesha wanaochukua masomo ya sayansi, hisabati na elimu ya msingi (kwenye msisitizo wa sayansi na hisabati), kupata mikopo ya elimu, nafasi iliyoanza kutumika mwaka 2014, lakini hatua hiyo ilisimamishwa wakati wa muhula wa masomo wa mwaka 2016/17.

Hata hivyo, HESLB ilikaririwa ikisema kwamba maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ililenga kutekeleza maagizo ya serikali. Hata hivyo, jana Profesa Ndalichako alisema kwamba uamuzi wa kusimamisha mikopo hiyo,ulitokana na nia ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la sayansi pekee.

“Mwaka 2004 tuliingiza diploma, lakini kwa masomo ya sayansi pekee sasa, tunataka kuwa na kipengele kinachopanua wigo ili tuweze kuhusisha kozi nyingine za diploma ambazo zinaenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa,” alifafanua waziri huyo.

Kwa mwaka wa masomo 2016/17, serikali ilipanga bajeti ya Sh bilioni 483 ambazo zitakopeshwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Katika mwaka huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo walikuwa ni 25,715.

Wakichangia mjadala huo, Mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF) alitahadharisha kuhusu vipaumbele vya kitaifa na kutaka kuwapo na ufafanuzi ili kuondoa utata. “Sijafurahi sana na phrasing of national priority.

Naogopa isije ikajibana au ikatumika katika hali itakayoleta utata. Hivi karibuni tulikuwa na utata mkubwa wa nani apewe mikopo…sasa tunasikia kuwa tunaenda kwenye uchumi wa viwanda isije fedha zote zikapelekwa kule.

“Kutafutwe njia ya kudetermine hizo priority za kitaifa na kujua watakuwa wangapi ili tujue kichumi itagharamu kiasi gani ilitusishindwe huko mbele,” alisema Saleh.

Fikra ya kutanua wigo kwa wanafunzi wa Stashahada ilifafanuliwa na watu wa Bodi ya Mikopo kwamba imezingatia kuwa katika sekta zote kutatakiwa uwiano wa wataalamu wa kada mbalimbali. Aidha, imeelezwa kuwa waziri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wataweza kushauriana na kuona hitaji ya kada mbalimbali zinavyokwenda.

Chanzo: HabariLeo

MATOKEO KIDATO CHA PILI (FTNA) NA DARASA LA NNE (SFNA) 2016

examresults

Fuata viunganishi hapo chini

Kidato cha Pili 2016

Darasa la Nne

MHADHIRI WA CHUO KIKUU AKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA YA NGONO

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni inamshikilia Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (66) kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kike baada ya kumwekea mtego kwa lengo la kumpa alama nzuri katika mtihani wake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ijumaa hii, Kaimu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Dennis Manumbu, alisema awali mwanafunzi huyo alitoa taarifa ya kuombwa rushwa ya ngono na Mahimbo ili ampatie matokeo mazuri ya mtihani wa marudio (Supplementary Examination) alioufanya Januari 5, mwaka huu.

“Amekamatiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyopo mwenge Mlalakuwa Dar es salaam, siku ya Alhamisi tarehe 12 mwezi wa kwanza mwaka 2017 majira ya alasiri. Mtuhumiwa bwana Mahimbo alikamtwa na Takukuru baada ya kuwekewa mtego kufuatia na taarifa iliyotolewa na mwanafunzi aliyekuwa akiombwa rushwa hiyo ili aweze kumpatia matokeo mazuri ya mtihani wa marudio,” alisema

“Natoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Takukuru ili kuweza kuzuia vitendo vya rushwa na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao uchunguzi utathibitisha kukabiliwa na tuhuma za rushwa ikiwamo rushwa ya ngono”.

Aidha Manumbu alisema rushwa ya ngono ni kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na Kupambana na rushwa inayoeleza kuwa ni kosa kwa mtu kutumia mamlaka aliyonayo kumtaka mtu kimapenzi ili ampe upendeleo katika kumhudumia.

Chanzo: PressTZ

%d bloggers like this: