Home » Habari » UZALENDO WA MWALIMU NYERERE JUU YA PESA ZA UMMA ZILIZOTUMIKA KUMSOMESHA MAKERERE UNIVERSITY

UZALENDO WA MWALIMU NYERERE JUU YA PESA ZA UMMA ZILIZOTUMIKA KUMSOMESHA MAKERERE UNIVERSITY

Advertisements

mwalimu-kambarage

Tukiwa tunatimiza miaka 17 ya kifo cha mwasisi wa taifa letu, hayati Mwalimu Julius K. Nyerere aliyefariki dunia tarehe 14/10/1999, kama taifa tuna mengi ya kujifunza na kuyaenzi juu yake.

Leo kupitia mtandao huu wa Elimu Tanzania, tujikumbushe hisia za Nyerere juu ya pesa za Umma zilizotumika kumsomeshea chuo kikuu Makerere kama ilivyonukuliwa hapo chini.

“..Wakati nikiwa Makerere, niligundua kwamba serikali ya nchi yangu
ilikuwa ikinilipia kiasi cha paundi 80 kila mwaka kwa ajili ya elimu
yangu. Lakini hio haikuwa na maana kubwa sana kwangu, isitoshe paundi
80 ni chembe ndogo tu ya kiasi cha jumnla ya pesa zinazokusanywa na
kutoka kwa walipa kodi wa nchi yangu, yaani wa-Afrika. Leo hii, paundi
80 ziimeongezeka thamani yake na kuwa na maana kubwa kwangu. Siyo
kwamba ni zawadi muhimu tu na tunu kwangu, lakini pia ni deni ambalo
kamwe sitaweza kulilipa.”

“Sina uhakika kama wengi wetu wamepata kufikiria kwamba wakati paundi
80 zilikuwa zinatumika kunitunza mimi kule Makerere, hela hizo
zingeweza kujenga Zahanati angalau mbili katika kijiji changu au
chochote kingine Tanzania.”

“.. Inawezekana kabisa kuwa wananchi walikuwa wanakufa kwa ukosefu wa
dawa kwa sababu tu ya kukosa paundi zile 80 zilizokuwa zikilipwa kwa
ajili yangu. Kwa hiyo kuwapo kwangu chuoni kuliinyima jamii huduma ya
wale wote ambao wangeweza kusomeshwa kwenye shule chini ya miti, na
kuwaandaa kina Aggreys na Booker Washingtons, Je nitawezaje kamwe
kutolilipa hilo deni kwa jamii yangu hii?.”

“Jamii inatumia fedha zote hizo kwa ajili yetu kwa sababu inataka tuwe
nyenzo za kuiinua jamii hiyo. Kwa hiyo lazima siku zote tubakie chini
ya jamii hiyo na kuhimili uzito wote wa wananchi ambao wanahitaji
kuinuliwa, na lazima tusaidie kuifanya hiyo kazi ya kuwainua wananchi
wasiojiweza”

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: