Home » Habari » Stori yote ya walimu kumjeruhi mwanafunzi iko hapa, mawaziri wachukua hatua kali

Stori yote ya walimu kumjeruhi mwanafunzi iko hapa, mawaziri wachukua hatua kali

Advertisements

Habari iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii leo ni juu ya ukatili uliyofanywa na walimu wa mafunzo dhidi ya mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa Mbeya.

Ukweli wa tukio:

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu ambao ni Frank Msigwa kutoka DUCE, ambaye ndiye chanzo kikubwa kufuatia madai ya mwanafunzi huyo kugoma kufanya adhabu aliyopewa na mwalimu huyo. Wengine ni John Deo na Sante Gwamoka kutoka DUCE,mwingine ni Evans Sanga kutoka Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, wote wakiwa mafunzoni.

Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video.

Hatua zilizo chukuliwa hadi sasa:

1.Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba:

Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.

2. Waziri wa Tamisemi, Simbachawene:

Ninaagiza mamlaka husika za kinidhamu kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya Kutwa Mwl. Magreth Haule, avuliwe madaraka kutokana na kukaa kimya huku kukiwa na tukio la unyama dhidi ya mwanafunzi.

walimu waliohusika na tukio hilo ni wa mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo walishirikiana kumshambulia mwanafunzi huyo.

3. Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amosi Makala:

Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu na mwalimu mkuu kwa mahojiano, kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu na mwanafunzi aliyepigwa.

Nawahakikishia serikali itawasaka popote walipo walimu hawa waliofanya tukio hili na kufikishwa ktk vyombo vya dola na sheria.

Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibabu.

4. Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako:

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Ndalichako amewafukuza chuo walimu waliohusika na kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya kutwa Mbeya.

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: