Home » Uncategorized » Kioja: Mzazi feki achapwa viboko

Kioja: Mzazi feki achapwa viboko

Advertisements

14257598_1491194204227956_4555863469686570246_o

14188420_1491194164227960_83337613388976978_o

Mkuu wa Shule moja ya Sekondari hapa nchini ameamua kutoa adhabu kali ya viboko kwa Dada mmoja ambaye aliletwa shuleni hapo na mmoja wa wanafunzi aliyetakiwa kuita mzazi wake akijifanya kuwa yeye ndiye Mama Mzazi wa Mwanafunzi huyo.

“Mzazi Fake” huyo alipofika shuleni hapo alikutana na Waalimu ambao walimtilia mashaka kuwa sio Mzazi halisi. Walipoamua kumuuliza maswali kadhaa kuhusu maendeleo na historia ya mwanafunzi huyo Mzazi huyo hakuwa anajua lolote kuhusu mwanafunzi husika na hivyo wakabaini kuwa sio mzazi halisi bali aliokotezwa njiani ili aje shuleni kumtetea mwanafunzi huyo.

Walimu ili kujiridhisha waliamua kufanya mawasiliano na wazazi halisi wa mwanafunzi huyo kupitia kitabu cha kumbukumbu za mawasiliano ya wazazi zilizopo shuleni hapo na kubaini kuwa wazazi halisi hawajui lolote kama mtoto wao amefanya makosa shuleni na kwamba anatakiwa aende na mzazi wake. Pia wazazi halisi walikana kumfahamu Dada aliyejitokeza shuleni hapo akidai kuwa ndio mzazi wa mwanafunzi huyo. Dada huyo alipobanwa zaidi alikiri kuwa sio mzazi halisi na kwamba alichukuliwa mtaani tu ili aje amtetee shuleni.

Ndio uongozi wa Shule hiyo ulipoamua kugonga kengele na kukusanya wanafunzi wote kisha Mwalimu Mkuu akaamua kutoa adhabu kali ya viboko 6 kwa “mzazi fake” badala ya mwanafunzi mbele ya umati wa wanafunzi wote shuleni hapo ili iwe fundisho kwa wengine.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya “mzazi fake” kukubali kucharazwa viboko mbele ya wanafunzi badala ya kupelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka, yeye akaamua ni heri acharazwe viboko ili yaishe.

Adhabu imetekelezwa na iwe fundisho kwa wengine.

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: