Home » 2016 » September

Monthly Archives: September 2016

Advertisements

MSIKILIZE MWALIMU NYERERE AKIHOJIWA JUU YA ELIMU MIAKA YA 1960

Advertisements

HIVI NDIVYO VYUO VIKUU BORA DUNIANI

Chuo kikuu cha Oxford Uingereza
Chuo kikuu cha Oxford Uingereza

Chuo kikuu cha Oxford kimeibuka kidedea katika orodha ya vyuo vikuu bora duniani ya Times Higher Education. Hi ni mara ya kwanza kwa chuo kikuu cha Uingereza.

Oxford imeisukuma katika nafasi ya pili, California Institute of Technology, ambayo imekuwa ikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliopita .

Katika orodha ya vyuo vikuu bora barani Afrika, chuo kikuu cha Cape Town kimeibuka wa kwanza kutoka Afrika kusini kwenye orodha hiyo ya Times Higher Education.

Inadhihirisha umahiri wa taifa hilo, ambalo vyuo vyake vikuu 6 vipo katika nafasi za vyuo vikuu 15 bora kikwemo chuo cha Witwatersrand katika nafasi ya pili, Stellenbosch nafasi ya tatu, tChuo kikuu cha KwaZulu-Natal katika nafasi 5 na chuo kikuu cha Pretoria katika nafasi ya sita.

Chuo kikuu cha Makerere
Chuo kikuu cha Makerere

Makerere kilichopo Uganda ndiyo chuo kikuu nje ya Afrika kusini kufanikiwa kuwa atika nafasi ya nne.

Vyengine ni chuo kikuu cha Ghana katika nafasi ya 7, na chuo kikuu cha Nairobi katika nafasi ya 8.

Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama mafunzo, utafiti, na mtazamao wa kimaaifa – kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika – Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana – “zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti” nchini mwao na vimeshuhudia “ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita”.

Chanzo: BBC

JPM AFANYA UTEUZI HUU KWENYE SEKTA YA ELIMU

magufuli3

Jana, September 19 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Prof. Jacob Philip Mtabaji kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuanzia tarehe 15 Septemba, 2016.

Prof. Jacob Philip Mtabaji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Awadhi Mawenya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Kamisheni ya TCU kuvunjwa.

Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Mathew L. Luhanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016. Prof. Mathew L. Luhanga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Daniel Mkude ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016. Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.

Nne, Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudensia M. Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016. Gaudensia M. Kabaka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Augustine Mahiga ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Tano, Rais Magufuli amemteua Mariam Mwafisi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia 05 Septemba, 2016. Mariam Mwafisi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Deogratias Ntukamazina ambaye amemaliza muda wake.

NAFASI ZA KOZI ZA KIINGEREZA UBALOZI WA UINGEREZA

british-council-tanzania

14368896_1018101714954920_6783435921841701929_n

BODI YA MIKOPO YAZUNGUMZA JUU YA TOZO YA 6% KWA WANUFAIKA WA MIKOPO

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu pamoja na kwamba inatoa mikopo kwa wanafunzi haitozi riba katika marejesho ya mkopo huo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya                                 Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa

Akizungumza Jijini Dar es salaam katika KIKAANGONI ya EATV, Mwaisobwa amesema kwamba Bodi ya Mikopo inachokifanya kwa walipaji ni kutoza tozo ya kulinda thamani ya mkopo ambao mnufaika alichukua.

‘Tunatoza kiwango cha asilimia 6 ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo kiwango ambacho ni tofauti kabisa na riba, ukiangalia benki kwa sasa hivi kuna ambazo zinatoza zaidi ya asilimia 20 hivyo sisi kazi yetu tunasaidia kutoa elimu na siyo kunufaika zaidi” Amesema Mwaisobwa.

Aidha Mwaisobwa amesisitiza kwamba kwa wote ambao walichukua mikopo na wanajificha kukwepa kulipa, ni lazima watalipa kwa kuwa uhakiki kwa sasa hivi unafanyika katika maeneo mbalimbali na wakibainika penati ya asilimia 10 itawahusu wote wanaokwepa na kuongeza kwamba wanaojitokeza kulipa kwa hiari watatozwa asilimia 8% ya pato lao kwa mwezi.

Pamoja na hayo bodi hiyo imewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutambua kwamba fedha zinazotakiwa kulipwa ni zote kuanzia za chakula, ada pamoja na fedha za mafunzo kwa vitendo.

Chanzo: EATV

%d bloggers like this: