Home » Matangazo » NACTE waongeza mda wa maombi ya kusoma Cheti na Diploma. Ipo pia orodha ya vyuo vyenye nafasi hizo

NACTE waongeza mda wa maombi ya kusoma Cheti na Diploma. Ipo pia orodha ya vyuo vyenye nafasi hizo

Advertisements

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

NACTE LOGO

Baraza linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa muda wa nyongeza wa kutuma maombi kwa mwaka 2016/2017 umeongezwa hadi tarehe 13 Agosti 2016 ili kuruhusu ambao hawakukamilisha maombi yao kuyamaliza na ambao hawajafanikiwa kuomba kutuma maombi yao.


Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu pia baraza linashauri waombaji wajipime na kuangali ushindani wa kozi ili kufanikisha kuchaguliwa kwao. Vyuo na kozi zilizo na nafasi zimeainishwa hapa.


Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.


Baraza pia linapenda kuwataarifu waombaji waliokwisha chaguliwa kwenye awamu ya kwanza na wanataka kuomba uhamisho kutoka kozi ama chuo kimoja kwenda kingine wavute subira utaratibu utatolewa mara tu majibu ya waombaji wa awamu ya pili yatakapotolewa.


Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.


Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 08th Agosti, 2016

Advertisements

16 Comments

 1. baraka ndunguru says:

  mm n muitimu wa kidato cha nne na nmepata pass tano ambazo ni historyC civicsD biologyD kswhlD na englishD naomba ushauli nikasome chuo gan

  Like

 2. eviana mgalula says:

  nlipenda kuuliza kwa sisi tulio malza fom6 na principal pass 2 tuna sifa ya kujiunga na diploma ya ualimu wa sekondary?

  Like

  • Elimu Leo says:

   Principal pass 2 hata degree unasoma

   Like

   • Nyely wapy says:

    Kama umemaliz form 4 ukaaply diploma ya nursing na unavigezo vyote lakini kwa kuhofia ushidani utakuwa mkubwa ukaamua kuaply mala ya pili vyuo vya private unaluhusiwa kuaply kupitia nacte zaidi ya mala moja at the same year

    Like

 3. kimu says:

  napenda kuulzia kwamba Mimi ni muhitim form four na ninahitaji kusomea IT chuo kilichopo dar kiitwacho kitm ningeomba kujua naweza kukubaliwa na nacte kusomea kwa ngazi ya cheti na baada ya hapo diploma lakn ninafour ya 28/na ningependa kujua garama ndugu zangu

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Sifa za kusoma certificate ni ufaulu wa kuanzia D nne na kuendelea. Kuhusu ada ni vyema ukawasiliana na chuo husika

   Like

 4. Laudato si says:

  Nina Weza Kupata Form Ya Chuo Cha Afya Kupitia Website Yenu

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Hatutoi form ya chuo chochote wala kupokea malipo yoyote, msaada wetu kwako ni kukuunganisha na chuo pale ambapo NACTE watakuwa wametangaza rasmi kufungua mfumo wa udahili. Taratibu zingine zote utazifanya wewe na chuo husika.

   Like

 5. aneth john says:

  Nina biology D,na chemistry D,na phyisics F je naweza kusoma course gani ?naomba mnisaidie

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Kama jumla ya ufaulu wako ikiwemo na masomo mengine ambayo hukuyataja hapa inafikia jumla ya D nne au zaidi, unaweza kusoma kozi za afya.

   Like

 6. Mm nilichaguliwa chuo ambacho ni private ila sikuweza kuripoti kwa sababu za kiuchumi na nilitaka kubalisha chuo lakn mda ukawa umeisha sasa tayari nimeshatuma barua ya kuahirisha mwaka wa masomo na kuomba ni pangiwe chuo cha serikal mwaka wa masomo 2017/2018 hivyo naombeni nacte mnisaidie kama ushauri na mwongozo niliopewa kama ni sahihi

  Like

 7. maria lotary Ndunguru says:

  naitaji kuuliza sifa za kujiunga chuo cha uwalimu mwaka 206/17 ni zipi? naombeni mnijibu

  Like

 8. maria lotary Ndunguru says:

  naitaju kuuliza sifa za kujiunga uwalimu mwaka 206/17 ni zipi? naombeni mnijibu

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Sifa ni ufaulu wa D nne za olevel kwa ualimu wa grade A na ufaulu wa E moja ya advance kwa diploma ya ualimu. Kwa habari zaidi za kielimu, tufuate kwenye ukurasa wetu wa Facebook.

   Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: