Home » Habari » NACTE yatoa sababu na ushauri kwa wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na kozi za Cheti na Diploma walizoomba

NACTE yatoa sababu na ushauri kwa wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na kozi za Cheti na Diploma walizoomba

NACTE LOGO

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SABABU ZA KUTOKUCHAGULIWA KWA BAADHI YA WALIOOMBA KUDAHILIWA

KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa kuna baadhi ya waombaji ambao hawakuchaguliwa kwenye uteuzi wa kwanza ambao ulitolewa tarehe 22 Julai 2016.


Mwombaji ambae hakuchaguliwa hupaswa kuangalia kwenye kurasa yake binafsi (profile) ili kupata sababu za kutokuchaguliwa. Sababu za kutokuchaguliwa zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Sifa za muombaji kuwa pungufu kulinganisha na sifa za chini za kozi;

2. Nafasi za mafunzo katika chuo na kozi husika kujaa kutokana na ushindani wa waombaji wenye sifa za juu zaidi.

3. Kutokamilisha ujazaji wa maombi kwenye mfumo;

4. Kutoambatanisha vyeti vya masomo kwa baadhi ya waombaji; na

Waombaji wanashauriwa kusoma kwa makini sababu hizo na kufuata ushauri unaotolewa ili kuweza kuchaguliwa katika uteuzi unaofuata.


Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu. Orodha ya kozi zilizojaa zimeainishwa hapa

.


Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.


Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 28 Julai, 2016


3 Comments

  1. Elina says:

    Ivi walisema selection tar.14inamana bado,na Kama Bado mpaka lini na taarifa inasema kuripot ni tar 25

    Like

  2. Nyely wapy says:

    Nina division 3 ya 22 phy D chem C bio C language C na mathematics D je? Nitachaguliw kwa vyuo vya serikali kujiunga na diploma ya nursing au clinical officer

    Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: