Home » Matangazo » Majina ya wadaiwa wa Bodi ya Mikopo kuwekwa hadharani wiki ijayo

Majina ya wadaiwa wa Bodi ya Mikopo kuwekwa hadharani wiki ijayo

Advertisements

index

Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: