Home » 2016 » July

Monthly Archives: July 2016

Advertisements

NACTE yatoa sababu na ushauri kwa wale ambao hawakuchaguliwa kujiunga na kozi za Cheti na Diploma walizoomba

NACTE LOGO

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU SABABU ZA KUTOKUCHAGULIWA KWA BAADHI YA WALIOOMBA KUDAHILIWA

KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za cheti na diploma na umma kwa ujumla kuwa kuna baadhi ya waombaji ambao hawakuchaguliwa kwenye uteuzi wa kwanza ambao ulitolewa tarehe 22 Julai 2016.


Mwombaji ambae hakuchaguliwa hupaswa kuangalia kwenye kurasa yake binafsi (profile) ili kupata sababu za kutokuchaguliwa. Sababu za kutokuchaguliwa zinaweza zikawa kama ifuatavyo:

1. Sifa za muombaji kuwa pungufu kulinganisha na sifa za chini za kozi;

2. Nafasi za mafunzo katika chuo na kozi husika kujaa kutokana na ushindani wa waombaji wenye sifa za juu zaidi.

3. Kutokamilisha ujazaji wa maombi kwenye mfumo;

4. Kutoambatanisha vyeti vya masomo kwa baadhi ya waombaji; na

Waombaji wanashauriwa kusoma kwa makini sababu hizo na kufuata ushauri unaotolewa ili kuweza kuchaguliwa katika uteuzi unaofuata.


Baraza linaomba ifahamike kuwa vyuo na kozi zilizojaa hazitaonekana tena wakati wa maombi bali kozi zitakazoonekana ni zile zenye nafasi tu. Orodha ya kozi zilizojaa zimeainishwa hapa

.


Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa punde uteuzi utakapokamilika. Waombaji wa vyuo hivi wanashauriwa kusubiri na kutokubadili machaguo yao hadi kutangazwa kwa uteuzi kwa vyuo vya Ualimu vya Serikali.


Aidha Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji wa Shahada ya Kwanza waliofanya maombi kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa Baraza kuwa utaratibu wa kukamilisha maombi yao utatolewa baada ya mashauriano kati ya Baraza na Tume ya Vyuo Vikuu yatakapokamilika.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 28 Julai, 2016

Advertisements

Majina ya wadaiwa wa Bodi ya Mikopo watakaochukuliwa hatua awamu ya kwanza

Accounting treatment for Bad Debt Recovered

The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB), hereby notifies all loan beneficiaries who are not servicing their loans and whose names appear herein that they have breached a contract as per the HESLB Act. No. 9 of 2004 (as amended) Section 19 (1).

These Loan Defaulters are further notified that according to HESLB Act No. 9 0f 2004 the Board, intends to take the following steps: –

(i) Shall be liable to legal action as per Section 19 (a) (1) of the HESLB Act.

(ii) Shall be subjected to additional monthly Penalty of 5% p.a. on the outstanding loans, over and above the 5% that was levied earlier.

(iii) Shall have his/her outstanding loan loaded with the cost of tracing that will be charged after being traced by the Board.

(iv) Shall be blacklisted and his/her information shall be submitted to the Credit Reference Bureaux, following which they shall be barred from access to credit facilities from all Financial Institutions.

(v) Shall be barred from securing Government scholarships or admission for Postgraduate studies in any Higher Learning Institution within and outside the country.

(vi) Their details shall be submitted to the Ministry of Home Affairs, Department of Immigration and all Embassies where they will be denied approval for travelling abroad.

All Loan Beneficiaries whose names have been published in the newspapers and on this website of the Board through http://olas.heslb.go.tz are required to repay their due loans immediately to avoid facing the above listed measures.  Loans statements and other details of their due loans can be accessed by visiting HESLB Offices or writing to:

Acting Executive Director,
Higher Education Students’ Loans Board,
P.O. Box 76068
Dar es Salaam
Email: info@heslb.go.tz

Find here the names >>>HESLB_DEFAULTERS_BATCH_1

Mbunge CHADEMA aingia darasani na kufundisha Hisabati

13775413_1148399351870148_1595435143897584124_n

Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA), Mh. Mwita Waitara ameendelea kufanya ziara katika shule mbalimbali za msingi jimboni humo akigawa vifaa mbalimbali ikiwemo madawati yaliyotolewa na serikali kufuatia agizo la Mh. Rais Dk. John P. magufuli la kutengeneza na kusambaza madawati kwa majimbo yote nchini ili kumaliza kabisa tatizo la watoto kukaa chini madarsani.

Akiwa shule ya msingi Magole, Waitara alipata pia fursa ya kuingia darasani na kufundisha somo la Hisabati pamoja na kufanya mambo mengine kama inavyoonekana katika picha.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Magole wakiwa wamebeba moja ya madawati waliokabidhiwa na Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara jana jijini Dar es salaam.
mwit2Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara, kulia akisalimiana na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kiboga iliyopo Chanika Mvuti Dar es Salaam wakati alipoenda kukabidhi msaada wa madawati jana
mwit3Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara, akizungumza na kina mama wa kikundi cha Kikoba Cha Mpanga wa Vikoba kilichopo Magole wakati alipokuwa akitembelea jimbo hilo jana
mwit4Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya msingi Magole wakati alipokabidhi msaada wa madawati
mwit5Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akimkabidhi msaada wa mipira Mwalimu wa Michezo, Emmanuel Zongo wa Shule ya Msingi Magole wakati alipokwenda kukabidhi msaada wa madawati jana
mwit6Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akizungumza na  na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbondole  baada ya kukabidhi madawati jana
mwit8Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kushoto, akimkabidhi msaada wa madawati kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbondole, Selemanai Mkombozi jana.
mwit9Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, akikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Msingi Magole jana.
Habari kwa hisani ya Mzee wa Mshitu

Kitabu cha muongozo wa kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka 2016/17

tcu-june1

Tume ya vyuo vikuu TCU imetoa kitabu cha muongozo wa kujiunga na vyuo vikuu nchini kwa mwaka 2016/17, kitabu hicho chenye taarifa kamili juu ya vyuo vyote nchini na taarifa nyinginezo za kuzingatia kabla hujatuma maombi yako kinapatikana katika link hii hapa chini

Undergraduare_Admission_Guidebook_2016_2017

Majina ya wadaiwa wa Bodi ya Mikopo kuwekwa hadharani wiki ijayo

index

Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

A/C No. 2011100205 – NMB
A/C No. 01J1028467503 – CRDB
A/C No. CCA0240000032 – TPB
Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

%d bloggers like this: