Home » Habari » NACTE yafunga kwa mda mfumo wa udahili wa pamoja

NACTE yafunga kwa mda mfumo wa udahili wa pamoja

Advertisements

th

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja unaoratibiwa na NACTE.


Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilisha mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki tatu hadi nne kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.


Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopenda kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.


Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa wazi na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.


Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kati ya wiki ya mwisho ya mwezi wa sita, 2016  na wiki ya kwanza ya mwezi wa saba , 2016.

Imetolewa na

Kaimu Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 7 Juni, 2016

Advertisements

2 Comments

 1. mjuni Faisal says:

  naomba nijue majina ya waliofanya udahili wa certificate na diploma kwa mda ulioongezwa na nacte majina yametoka

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Unaweza kuona jina lako kupitia Account yako uliyotumia kuomba nafasi. NACTE hawakutoa majina hayo hadharani. Rejea tangazo lao hapa chini
   Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi mbali mbali za cheti na diploma na Umma kwa ujumla kuwa uhakiki wa uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa cheti na diploma umekamilika na kwamba uteuzi huu sasa unaonekana kwenye kurasa binafsi (profile) za waombaji. Hii ina maana kuwa waliochaguliwa sasa wanaweza kuona mahali walipochaguliwa kupitia kurasa zao binafsi.
   Hata hivyo, Baraza linaomba radhi kwa kuwa uhakiki wa uteuzi kwa baadhi ya vyuo haujakamilika hivyo Baraza litashindwa kuwaonyesha waombaji wa vyuo hivyo uteuzi wao. Vyuo hivyo ni pamoja na vyuo vya kilimo na uvuvi na baadhi ya vyuo vikuu.
   Baraza pia linapenda kuwaarifu waombaji waliofanya maombi kwenye vyuo vya Ualimu vya Serikali kuwa uteuzi kwenye vyuo hivyo bado unasubiri mwongozo wa Serikali na hivyo watafahamishwa mara Baraza litakapopata mwongozo kutoka Wizara yenye dhamana ya Elimu juu ya uchaguzi huo.
   Imetolewa na
   Ofisi ya Katibu Mtendaji
   NACTE
   Tarehe: 10 Septemba, 2016

   Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: