Elimu Leo

Home » Habari » Bodi ya mikopo yakanusha habari hii ya uwongo

Bodi ya mikopo yakanusha habari hii ya uwongo

th (1)

KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016


Weka mawazo yako hapa