Home » Habari » Serikali kuwarudisha kazini walimu wa sayansi wastaafu

Serikali kuwarudisha kazini walimu wa sayansi wastaafu

Advertisements

Serikali ya Tanzania imesema kuwa katika kumaliza tatizo la walimu wa sayansi nchini serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa walimu wa masomo hayo lakini pia wataandaa utaratibu maalumu wa kuwarejesha walimu wastaafu wa masomo ya Sayansi.

 suleiman-Jaffo
 Naibu Waziri wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu wa Wizara ya TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa pamoja na utaratibu huo lakini pia wataandaa programu maalum ya kuwawezesha mbinu za kiufundishaji wahitimu wa elimu wa masomo ya sayansi ili kuwapa ajira.

Mhe. Jaffo amesema kwa sera ya ujenzi wa maabara kwa kila shule imeongeza changamoto ya hutaji wa walimu wa Sayansi hivyo kwa kufanya hivyo serikali itaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi.

Aidha Mhe. Jaffo ameongeza kuwa serikali imetoa miongozo katika halmashauri zote nchini kuhusu suala la uchangiaji wa ada katika mashule huku ikisisitiza kutoa kipaumbele kwa walimu wa sayansi wanaotafuta ajira.

Chanzo: EATV

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: