Home » Matangazo » Nafasi za masomo chuo cha serikali za mitaa

Nafasi za masomo chuo cha serikali za mitaa

Advertisements

374556_524888904188982_935758093_n

TANGAZO

NAFASI ZA MASOMO 2016/2017
Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kujiunga na masomo kwa ngazi ya Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) katika fani zifuatazo:-
• Local Government Administration
• Local Government in Accounting and Finance
• Community Development
• Human Resource Management
• Records, Archives and Information Management
• Procurement and Supply Management

SIFA
• Astashahada (Cheti)
Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne, mwenye ufaulu angalau kuanzia alama “D” nne.

• Stashahada (Diploma)
Mwombaji awe amehitimu kidato cha sita awe na ufaulu angalau kuanzia “Principal Pass” mbili na “Subsidiary” moja au awe na Cheti kutoka Chuo chochote kinachotambulika na serikali kwa ngazi ya Cheti, muda usiopungua mwaka mmoja.

Aidha, Chuo kinatoa mafunzo ya awali (Pre – Entry) kwa wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu angalau kuanzia alama “D” mbili au tatu ili kupata sifa ya kujiunga na ngazi ya Astashahada.

Chuo cha Serikali Mitaa kina Kampasi mbili; Kampasi Kuu Hombolo na Kampasi ya Dodoma mjini.
Kwa Kampasi Kuu Hombolo muhula wa masomo kwa mwaka 2016/2017 utaanza mwezi Agosti, 2016 na kwa Kampasi ya Dodoma Mjini muhala utaanza mwezi Oktoba, 2016.

Pia Chuo kinatoa kozi za muda mfupi (Short Courses) kutegemea mahitaji ya jamii.

Fomu za kujiunga na Chuo zinapatikana Kampasi Kuu Hombolo, Kampasi ya Dodoma Mjini na katika tovuti ya Chuo www.lgti.ac.tz

Advertisements

17 Comments

 1. Christine david says:

  Kama umepata ufaul wa d2 na c1 alafu umejisajili na mtihan kwa ajili ya kuongeza credit nyingine unaweza kujiunga na chuo huku unasubiri kufanya mtihani kwa alama iliyopungua

  Like

 2. maswi michael nyansoho says:

  naitwa maswi, naomba kuuliza muhula wa masomo 2018_19 unaanza lin

  Like

 3. mm naitwa omari zaharani Nina certificate ya local sasa nataka nijuunge na diploma hombolo meakani je usajili utakua mwezi gani ili nijipange vilivo

  Like

 4. Alhaji says:

  mimi ni mwanafunzi nilio hitimu kidato cha nne mwaka juzi alama zangu kwa ujumla nina D-5 na C2. baada ya kupata matokeo hayo nikajiunga na chuo cha TUMAINI makumira na kusomea IT CERT. na mpaka sasa nimemaliza cert. nataka nibadilishe course je kunauwezekano ….

  .

  Like

 5. Ally Nyakuti says:

  kwa wanaolipiwa na serikali,garama ya chakula na matibabu ni ya nani ?

  Like

 6. imma says:

  samahani, je naweza kuandika maombi kupiti kutumia mtandao

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Kwa sasa mfumo wa udahili wa NACTE bado haujafunguliwa, endelea kuwa nasi hadi watakapofungua mfumo huo utaweza kutuma maombi yako kwa mtandao

   Like

 7. justine says:

  naitaj nafas hapo chuon je nina kisw C English D hist D na bios D je nina sifa za kujiunga na chuo hicho na ni mwez gan mnapokea maombi na naomba ushauli pia ni koz ipi inaweza kunifaa na ajila zake ni za uhakika

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Unazo sifa za kusoma certificate chuo chochote kile, kuhusu kozi ni wewe uchague kipi unachokipenda . Udahili utatangazwa na mamlaka husika (NACTE), jiunge nasi upate taarifa kwa wakati.

   Like

 8. mimi ni afisa wa polisi na ninacheti cha polisi je naruhusiwa kujiunga na diploma kwa kutumia cheti hicho

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Tafadhali wasiliana na chuo husika kwa ufafanuzi zaidi au jaza form maalumu kwenye menu hapo juu kwa kubofya sehemu iliyoandikwa kutafuta chuo/shule

   Like

 9. chambo says:

  Mina D tatu naomba kujiunga na Chuo chenu
  0655064643 au pre entry

  Like

 10. bakari Issa says:

  naomba ufafanuzi wa gharama kwa ngazi ya Cheti

  Like

 11. boaz william says:

  Jaman mbona nacte hawajatoa matokeo yao sasa mpka sasa?!! Wakat ixhafahamik watu wanaenda colleg mwez oktob!!

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Ni kweli hawajatoa, na bado kwa kozi za Cheti na Diploma milango iko wazi kutuma maombi.
   Kama kawaida yetu tutawawekea hapa selection zote watakapokuwa wamekamilisha michakato yao

   Like

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: