Home » Matangazo » Taarifa kutoka NACTE kuhusu Diploma wanaotaka udahili wa degree

Taarifa kutoka NACTE kuhusu Diploma wanaotaka udahili wa degree

Advertisements

nacte-diploma-feb19-2013TAARIFA KWA UMMA

TAREHE 11 MACHI 2016

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuutangazia umma kuwa waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaoomba kujiunga na Shahada ya Kwanza zinazotolewa na  Vyuo Vikuu (Universities) au Vyuo Vikuu Vishiriki (Constituent Colleges of Universities) hawataweza kufanya hivyo sasa. Hii ni kwasababu Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) bado haijafungua rasmi Mfumo wa Udahili wa pamoja (CAS) unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)  na  Tume ya Vyuo Vikuu (TCU). Tume ya vyuo vikuu inatarajia kufungua mfumo huo wa kudahili kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza mara baada ya matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kuanzia  mwezi Mei 2016.


Hivyo basi, ikifika muda huo ndipo waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki kwa ajili ya kusoma Shahada ya Kwanza,  wataweza kuanza kuomba kudahiliwa kwa kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS).


Hata hivyo,  tunapenda kutoa taarifa pia kuwa kwa wakati huu, waombaji wenye Stashahada (Ordinary Diploma – NTA Level 6) wanaotaka kujiunga na Shahada za Kwanza zinazotolewa na  vyuo vya Elimu ya Ufundi au Taasisi zilizosajiliwa na Baraza (NACTE) waendelee kuomba kudahiliwa na Taasisi hizo kupitia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) unaoratibiwa na Baraza ambao umezinduliwa tarehe 4 Machi, 2016.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA UDAHILI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Advertisements

13 Comments

 1. Hashim Shaban says:

  mimi ni mhitimu wa stashahada ya elimu awali nataka niendelee na shahada na pia nataka mkopo nini vigezo vinavyo takiwa?

  Like

 2. Jose says:

  Unaweza kuaply mara mbili???

  Like

 3. Emmanuely yowely says:

  Mi ni muhitimu ualimu ngazi ya cheti grade ‘A’ nataka nijiunge kusoma open university diploma ,vp ni vigezo gani wanatumia kwa watu kama mimi kujiunga?

  Like

 4. jamani samahan naomba msaada wa kujua nina pass D mbili na c moja yani nina four ya point 31 baruhusiwa kuomba chuo kikuu naomba mnijibu kwa email yangu hii lukwandali15@gmail.com

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Kwa mujibu wa NACTE, kigezo kikuu cha kujiunga na chuo kwa ngazi ya certificate ni ufaulu wenye Pass 4 na pass inaanzia D hadi A. Kwa mujibu wa maelezo yako wewe una Pass 3, hata hivyo bado unaweza kutimiza ndoto yako kwa kuanza na kozi zingine kama vile NABE n.k

   Like

 5. William says:

  Nilituma maomba mwaka jana nikachaguliwa kusomea Community health lakin sikuweza kujiunga na Chuo niliyopangiwa kutokana matatizo binafsi Na nilipotaka kutuma tena kwa Mara nyngne mwaka huu nikaambiwa ulishajisajili mwaka jana, Nifanyaj ili niweze kutuma application?

  Like

  • Elimu Tanzania says:

   Ukishajisajili kinachofuata ni kuingia (log in) kwa kutumia utambulisho wako kila unapohitaji. Bila shaka ulichokifanya wewe ni kutaka kujisali tena ndo maana mfumo ukakugomea.

   Like

 6. lilian ambangile says:

  jamani mnatusaidiaje sisi ambao tumeshasoma diploma na tumepata gpa ya 3.3

  Like

 7. kusoma shahada anatakiwa awe na GPA ya ngapi kwa mhitimu wa level 6?

  Liked by 1 person

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: