Home » Habari » Wazazi mkoani Songea wasemekana kuwashauri watoto wao wavulunde kwenye mitihani

Wazazi mkoani Songea wasemekana kuwashauri watoto wao wavulunde kwenye mitihani

Advertisements

Uhaba-wa-madawati-620x308

Wakati serikali ikitangaza elimu bure kwa shule  za msingi na sekondari bado katika kata za Lilai na Muhukuru ambazo ziko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wazazi katika kata hizo wamekuwa wakiwaambia watoto wao waandike majibu yasiyo sahihi kwenye mitihanii ili wafeli huku wakifanya sherehe mtoto anapofeli mtihani wa darasa la saba na pia hutorokea Msumbiji serikali inapowafuatilia.

Hayo yamesemwa na  afisa tarafa wa tarafa ya Muhukuru iliyoko Songea mkoani Ruvuma Bi.Salma Mapunda wakati mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Benson Mpesya akizungumza na wananchi na walimu wa kata za Lilai na Muhukuru kuhusu sera ya serikali ya elimu bure.
Kutokana na hali hiyo mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Benson Mpesya ametangaza kuwachukulia hatu wazazi ambao watoto wao wamefaulu darasa la saba lakini hawajaripoti shule za sekondari  ilhali serikali imeondoa gharama kwa shule za msingi na sekondari.
Kwa upande wao wazazizi wanaoishi kata za Muhukukuru na Lilai mpakani mwa Tanzania na msumbiji wamesema ni kweli tabia ya kufurahia mtoto anapofeli ipo lakini kwa sasa imepungua kutokana na sera ya serikali ya elimu bure kwa shule za msingi
Chanzo: Radio One.
Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: