Home » Habari » Walimu waonywa kutokubeza elimu bure

Walimu waonywa kutokubeza elimu bure

Advertisements
unnamed-68Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ametangaza ‘vita’ dhidi ya walimu watakaobainika kutofundisha kwa wakati darasani kwa kisingizio cha mpango wa Serikali wa elimu bure.

Mahiza alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao alichoitisha kwa ajili ya kuweka mikakati ya kikazi na wakuu wa shule, wakurugenzi wa halmashauri na maofisa elimu wa sekondari mkoani Tanga.

Alisema baadhi ya walimu katika shule za msingi na sekondari wamekuwa wakitegea kufundisha na wanapofuatwa na wanafunzi huwajibu hiyo ndiyo elimu bure. “Wanawaambia wanafunzi subirini tu mtaisoma namba mwaka huu,” alisema Mahiza.

Alisema lugha hizo za kuwasimanga wanafunzi ni sawa na kuidhalilisha Serikali jambo alieleza kuwa hatakubali litokee tena.

“Nitawaweka kizuizini walimu watakaotegea au kubainika kutoa lugha za kuitusi Serikali kuhusu mpango wa elimu bure, nitatumia Sheria Namba 8 ya Usalama ya Mwaka 2010 kwani huko ni kuhujumu elimu,” alisema Mahiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene alisema Serikali imetenga Sh131.4 bilioni ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.

Alisema Serikali imejipanga kugharamia uendeshaji wa shule ili kuziba pengo la ada na michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wazazi na walezi.

Habari kwa hisani ya Mwananchi Publishers
Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: