Home » Habari » Chuo kikuu cha Ushirika Moshi chapata Makamu mkuu wa kwanza tangu kipandishwe hadhi na kuwa chuo kikuu kamili

Chuo kikuu cha Ushirika Moshi chapata Makamu mkuu wa kwanza tangu kipandishwe hadhi na kuwa chuo kikuu kamili

Advertisements

Mkuu wa chuo kikuu cha ushirika Moshi Mh. Pius Msekwa amemteuwa Prof. Faustine Karrani Bee kuwa Makamu mkuu wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka mitano kuanza mwezi Novemba 2015.

Uteuzi huo umefanyika kwa kuzingatia sheria ya vyuo vikuu No.7 ya mwaka 2005 na mkataba wa uanzishwaji chuo hicho wa mwaka 2015 pamoja na sheria zake za mwaka 2015

  •  Matukio katika Picha kwa hisani ya ofisi ya Makamu mkuu wa chuo kikuu cha ushirika, Moshi.12657977_1036074069796904_1141822747062634259_o Makamu mkuu wa chuo kikuu cha ushirika Moshi, Prof. Faustine Bee.12513678_1036074573130187_3083847591760356655_o Kutoka kushoto ni Prof. Chambo (nywele nyeupe), Prof. Donge na Mr. Mhandeni. Prof. Chambo ni mkuu mstaafu wa kilichokuwa chuo cha ushirika na baadaye chuo kikuu kishiriki.12694635_1036074816463496_6260385776663715651_o12672021_1036074833130161_889985771968774944_o12622225_1036074509796860_7923169517420843669_o12633641_1036074489796862_2918640804790856437_o

Prof. Bee ni msomi mwenye shahada za Uzamivu na Uzamili katika maendeleo na shahada ya kwanza katika uchumi. Amechapisha na kufundisha katika chuo hicho kwa mda wa miaka 28 tangu kilipokuwa chuo cha Ushirika baadaye chuo kikuu kishiriki cha ushirika na stadi za biashara (MUCCoBS) na sasa ni chuo kikuu kamili cha ushirika Moshi (MoCU).

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiutawala katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na:

Kaimu makamu mkuu wa chuo – Sept 2014 hadi Nov 2015

Mkuu wa chuo kikuu kishiriki – April 2010 hadi Sept 2014

Naibu mkuu wa chuo (Taaluma) – 2009 hadi 2014

Kaimu naibu mkuu wa chuo (Taaluma) – 2007 hadi 2009

Nyadhifa zingine ni:

Mkurugenzi, utafiti na Huduma za ushauri – 2000 hadi 2007

Mkuu wa idara, Huduma za ushauri – 2000.

Prof. Bee anakuwa mtu wa kwanza kushika wadhifa wa makamu mkuu wa chuo hicho tangu kipandishwe Hadji na kuwa chuo kikuu kamili mwezi septemba 2014. Ameoa na ana watoto kadhaa.

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: