Home » Habari » Mavazi ya walimu wa kike ni tatizo kwa maadili – Mkuu wa wilaya.

Mavazi ya walimu wa kike ni tatizo kwa maadili – Mkuu wa wilaya.

Advertisements

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Bituni Msangi amesema kuwa baadhi ya walimu wa kike nchini hawavai mavazi yenye maadili ya ualimu hatua ambayo huwasababisha wanafunzi hasa wa kiume kuwataka kimapenzi.

Msangi ambaye pia kitaaluma ni mwalimu ametoa kauli hiyo kwenye hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Walimu (CWT) Wilayani Kongwa kwa ajili ya kuwaaga walimu waliostaafu katika Wilaya hiyo.

Amesema kuna baadhi ya walimu wa kike ambao wamekuwa wakikiuka maadili kwa kuvaa mavazi mafupi na ya kubana wawapo kazini hali ambayo huwa inawanyima wanafunzi wa kiume utulivu wa kujifunza ambapo amewaagiza maofisa elimu kuwaeleza walimu wao namna bora ya uvaaji.

Katika hafla hiyo jumla ya walimu 17 waliostaafu walipata zawadi ya mabati 20 kila mmoja waliyopewa na chyama cha walimu Wilayani humo.

SOURCE: EATV.


Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: