Home » 2016 » February

Monthly Archives: February 2016

Advertisements

Hizi ndo juhudi za DC Paul Makonda kutatua kero ya usafiri kwa walimu wa Kinondoni

  • imagesMkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Paul C. Makonda (Picha na maktaba yetu)

Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wakizungumza na wanahabari, wamesema walimu
watatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.
Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.
Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.

Je, unadhani hatua hii itasaidia kuwaondolea usumbufu walimu hao?

Advertisements

Hizi ndo shule 10 bora kwa kidato cha nne mwaka 2015 na ada zao

2.feza+girls


“Usione vyaelea vimeundwa”, huo ni msemo wa wahenga ukimaanisha kila mafanikio yana maandalizi.

Msemo huo unaendana na kilichotokea katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita, ambapo katika shule 10 zilizofanya vizuri hakuna hata moja yenye maandalizi hafifu. Shule nyingi kati ya hizo ada zake ni kuanzia Sh8 milioni hadi tisa kwa mwaka.

Uchunguzi wetu umebaini kuwa shule hizo zote ni zenye majengo mazuri, walimu wazuri na wenye motisha, maabara zilizokamilika sehemu nzuri za kulala na zinazotoza ada zaidi ya Sh2.5 milioni, mbali ya gharama nyingine za chakula, malazi na vitabu.

Shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizoshika nafasi za kwanza ni Kaizirege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls (Mbeya), Alliance Boys ya Mwanza, Canossa (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Alliance Rock Army (Mwanza), Feza Girls na Feza Boys (Dar es Salaam) pamoja na Uru Seminary (Kilimanjaro) ambayo ada yake imetajwa kati Sh1.5 milioni au Sh1.6 milioni kwa mwaka .

Uchunguzi huo umebaini shule tano kati ya 10, zilizoongoza ada zake ni kuanzia Sh8 milioni hadi tisa kwa mwaka.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kaizirege iliyoshika nafasi ya kwanza, kila mmoja analipa Sh2.5 milioni za ada. Malipo yote hayo kwa shule zote 10 ni tofauti na gharama za malazi, chakula na vitabu ambavyo malipo yake yanajitegemea.

Kwa makadirio ya ada pekee, mwanafunzi atakayesoma shule hii kwa miaka minne endapo ada hiyo haitaongezeka, atapata elimu hiyo bora katika mazingira mazuri ya kufundishia, lakini lazima awe na Sh10 milioni.

Meneja wa shule hiyo, Eulogius Katiti alisema wanafunzi wanasoma katika mazingira bora, sehemu nzuri ya kulala, chakula bora, vifaa vyote vya kufundishia na hakuna somo linalosomwa kwa nadharia, yote husomwa kwa vitendo kama inahitajika kufanya hivyo.

“Angalia kwenye mtandao, utaona ubora wa mazingira ya shule, mabweni, jumlisha na matokeo ya mwisho ndiyo utaona ni kwa jinsi gani fedha yao inafanya kazi na kuwapa kilicho bora,” alisema Katiti.

Shule ya wasichana ya St. Francis iliyopo mkoani Mbeya, iliyoshika namba tatu, ili mwanafunzi ajiunge na shule hiyo, anatakiwa alipe ada ya Sh2.2 milioni kwa mwaka, huku akitakiwa kulipa katika mikupuo minne.

Mwanafunzi anayesoma katika shule hiyo, anatakiwa kulipa kiasi cha Sh8.8 milioni kwa miaka minne (endapo ada itabaki palepale) mbali ya kulipia bweni, vitabu, chakula na malazi.

Katika Shule ya Sekondari ya wasichana Canossa ya Dar es Salaam, mzazi anahitaji kuwa na Sh3 milioni, ili mwanaye asome mwaka mmoja shuleni hapo, zikiwamo gharama za malazi, chakula, vifaa vya kusomea na ada.

Kwa maana hiyo kwa miaka minne anatakiwa kuwa na kiasi cha Sh12 milioni ili aweze kusoma shule ya Canossa.

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Feza Boys ada ni Sh2.9 milioni, lakini ikijumlishwa na gharama za chakula, malazi na vifaa vya masomo, jumla inafika Sh8 milioni na ushehe, ikiwa ni chini kidogo ya Sekondari ya Feza Girls ambazo gharama yake inafikia Sh9 milioni kwa mwaka.

Mkuu wa taaluma wa shule hiyo, Zakia Irembe alitetea gharama hizo, akisema zinaendana na kiwango cha elimu anachopata mwanafunzi na utulivu anaokuwa nao awapo shuleni hapo.

Alisema hakuna kitu kigumu katika masomo kama kusoma huku mwanafunzi anawaza atakula nini, hana uhakika wa kulala, lakini kwao chakula bora, malazi ya kuvutia, uhakika wa kufanya vizuri kutokana na weledi wa walimu katika kufundisha ndiyo siri pekee ya mafanikio yao.

Irembe alisema katika mlo wa wanafunzi kila wakati lazima kuwe na matunda, huku wanafunzi hao wakiwa hawali ugali na kufua nguo ni uamuzi wa mwanafunzi ama atumie mikono au mashine, uhakika wa umeme, kamera za CCTV kwa ajili ya usalama na kila bweni lina eneo la kupumzikia kutizama taarifa ya habari.

“Mzazi analipa fedha anabaki anatudai elimu, jukumu la kusimamia chakula, malazi ni letu, ndiyo maana vitu vyote kwetu ni bora ili kupata elimu bora pia. Elimu inahitaji uwekezaji mkubwa, kusoma siyo kila mtu anaweza, kunahitajika vitu vya ziada kuhakikisha akili ya msomaji inawaza masomo pekee,” alisema Irembe.

Mwanafunzi aliyeshika namba moja katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu, Butogwa Shija aliyekuwa akisoma katika Shule ya Wasichana Canossa, alisema kuwa licha ya kupenda kusoma, mazingira mazuri ya kusomea, uhakika wa kupata kila anachotaka katika kujifunza ndiyo chachu ya mafanikio yake.

Mzazi wa mwanafunzi Innocent Lawrence aliyeshika nafasi ya tatu katika mtihani huo kutoka Feza Boys, Lawrence Nyakabunda alisema kuwa ada anayolipa katika shule hiyo inalingana na elimu anayopata mwanaye.

Alisema anakubaliana na ada kuwa kubwa, lakini anaridhishwa na kiwango cha elimu kijana wake anachopata.

Wakati wenye shule na wazazi wakisema hayo, Msomi wa masuala ya elimu, Profesa Kitila Mkumbo alisema sababu kubwa ya shule hizo kufanya vizuri ni aina ya wanafunzi wanaochukua, wanakuwa wamechujwa hadi wanapofika katika mtihani wa mwisho wote wanakuwa bora.

Alisema shule hizo pia zina walimu wa kutosha, wenye weledi wa ufundishaji, huku wakipewa motisha ya kufanya kazi hiyo.

Chanzo: Mwananchi

(more…)

Wanafunzi wa shule ya sheria watinga wizarani kudai mikopo

images

Akizungumza mara baada ya kutoka katika ofisi hiyo, mwenyekiti wa wanafunzi hao Wellwel Steven amesema kuwa wamekuwa wakiishi kwa kubahatisha shuleni hapo baada ya bodi kubadilisha mfumo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi hao.

Bw. Steven amesema kuwa utaratibu wa awali ulikuwa ni kwamba wakiingia katika shule hiyo ya sheria walikuwa wakipewa ruzuku ya kujikimu wenyewe lakini baada ya kuingia wao ambao ni court ya 20 walibadilishwa kuingia kwenye mfumo wa kunufaika na mikopo ya elimu ya juu.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa baada ya kubadilishwa kwa mfumo huo wengi wameonekana hawana vigezo vya kupata mikopo hiyo, hivyo wamefika katika ofisi hiyo kwa kuwa wengi wao wameathirika na mfumo huo ambao zamani walikua wanapata ruzuku serikalini na sasa wanatakiwa kufikia vigezo ili kupata mikopo toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo kaimu mkuu kitengo cha habari na mawasiliano Bi. Farida Khalfani amesema kuwa wanafunzi hao hawajafauta uratibu ambao wanatakiwa kufanya ikiwemo kukata rufaa ikiwa hawajapata mikopo lakini wao wamechukua jukumu la kufika moja kwa moja katika wizara hiyo.

Bi. Farida ameongeza kuwa wizara hiyo wala shule yenyewe ya sheria (Law School) haihusiki na utoaji wa mikopo hiyo, na kusema kuwa wizara iliingilia kati kuhusiana na utoaji wa ruzuku kipindi cha nyuma kwa kuwa sheria za mwanzo zilikuwa hazijaweka bayana juu ya upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi hao.

Chanzo: EATV

Kifahamu chuo cha kipekee Tanzania na Afrika: Hakihitaji ufaulu wa mitihani kujiunga, hakitoi vyeti kwa wahitimu, hakihitaji PhD kuwa mkufunzi.

PP2

SmartSuccess Universal College(SUCO) ni chuo cha mafunzo ya mafanikio katika Nyanja mbalimbali za kimaisha. SUCO kinamilikiwa na kampuni ya SmartMind & Partners. Kauli mbiu(motto) wa chuo hiki ipo katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza; kauli mbiu kwa Kiingereza  ni: “The University of success”, na kwa Kiswahili ni: “Chuo Kikuu cha Mafanikio”

Kwa habari zaidi ingia hapa

Matokeo ya Maarifa (QT) mwaka 2015

images

Yapo HAPA


 

%d bloggers like this: