Home » Mitihani » USAJILI WA CSEE NA QT KWA MWAKA 2016

USAJILI WA CSEE NA QT KWA MWAKA 2016

Advertisements

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2016 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba;

1. Kipindi cha usajili kwa watahiniwa wa Kujitegemea kitaanza tarehe 1 Januari, 2016 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT na kitaishia tarehe 29 Februari, 2016. Aidha watakaojisajili kwa kuchelewa yaani tarehe 01/03/2016 hadi tarehe 31/03/2016 watalipa Shilingi 65,000/= kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 40,000/= kwa watahiniwa wa mtihani wa Maarifa (QT) ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.

2. Mtahiniwa atakayejisajili kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2016 ni Yule ambaye anarudia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE); au amefanya na kufaulu Mtihani wa Maarifa (QT) katika kipindi kisichozidi miaka mitano (5) iliyopita; au mwenye sifa zinazolingana na hizo alizopata kutoka nje ya Nchi na kufanyiwa ulinganifu na Baraza la Mitihani la Tanzania.

3. Mtahiniwa atakayejisajili kufanya Mtihani wa Maarifa ni yule ambaye anatafuta sifa ya kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne kama mtahiniwa wa kujitegemea.

4. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada ya mtihani katika ofisi za Posta tu.

5. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya http://www.necta.go.tz kwani muda wa usajili hautaongezwa.
Imetolewa na:
KATIBU MTENDAJI
NECTA.

Advertisements

Weka mawazo yako hapa

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: